Toleo la 17 la mashindano ya Ulaya kwa ngazi ya timu za taifa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 14/06/2024 mpaka tarehe 14/07/2024 ambapo mwenyeji wa michuano hii ni nchi ya Ujerumani.

Ujerumani Magharibi iliandaa toleo la 1988, lakini hii itakuwa mara ya kwanza kwa Ujerumani kuandaa Mashindano ya UEFA ya Ulaya tangu kuungana tena. Kombe la Dunia la FIFA la 2006 pia lilifanyika katika nchi hiyo.

Katika michuano ya mwaka huu nchi zilizofuzu ni Germany, Scotland, Hungary, Switzerland,Spain, Croatia, Italy, Albania,Slovenia, Denmark, Serbia, England,Poland*, Netherlands, Austria, France,Belgium, Slovakia, Romania, Ukraine*, Türkiye, Georgia*, Portugal, na Czechia.

 

Makundi Yakoje?

Group A: Germany, Scotland, Hungary, Switzerland

Group B: Spain, Croatia, Italy, Albania

Group C: Slovenia, Denmark, Serbia, England

Group D: Poland*, Netherlands, Austria, France

Group E: Belgium, Slovakia, Romania, Ukraine*

Group F: Türkiye, Georgia*, Portugal, Czechia

 

Fainali ya UEFA EURO 2024 itachezwa wapi na lini?

Fainali itafanyika katika Uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin Jumapili tarehe 14 Julai 2024.

 

Viwanja Gani Vitatumika kwa ajili ya EURO 2024?

Viwanja kumi vilivyochaguliwa kuandaa mechi za mashindano haya ni pamoja na viwanja tisa vilivyotumika katika Kombe la Dunia la 2006 pamoja na Düsseldorf Arena.

Kwa kipekee, Munich Football Arena itakuwa ikiandaa mechi kwa mara ya pili mfululizo za EURO; uwanja wa nyumbani wa Bayern München ulikuwa moja ya viwanja 11 vilivyoandaa mechi wakati wa UEFA EURO 2020.

 

Viwanja vya wenyeji ni kama ifuatavyo ikiwa pamoja na idadi ya mashabiki wanaoweza kuingia:

 

Berlin: Olympiastadion Berlin (uwezo wa sasa: 71,000)

Cologne: Cologne Stadium (43,000)

Dortmund: BVB Stadion Dortmund (62,000)

Dusseldorf: Düsseldorf Arena (47,000)

Frankfurt: Frankfurt Arena (47,000)

Gelsenkirchen: Arena AufSchalke (50,000)

Hamburg: Volksparkstadion Hamburg (49,000)

Leipzig: Leipzig Stadium (40,000)

Munich: Munich Football Arena (66,000)

Stuttgart: Stuttgart Arena (51,000)

 

Tarehe muhimu za EURO 2024

Mashindano ya mwisho

14 Juni 2024: Mchezo wa ufunguzi wa UEFA EURO 2024, Munich Football Arena

14 Julai 2024: Fainali ya UEFA EURO 2024, Olympiastadion Berlin

 

Mascot wa EURO 2024 ni nani?

Mascot rasmi wa mashindano haya anaitwa Albärt kufuatia kura iliyopigwa na watumiaji wa UEFA.com na watoto wa shule kote Ulaya, kupitia mpango wa UEFA Football in Schools. Albärt, dubu mdogo wa kuchezea, alipata asilimia 32 ya kura. Mascot huyu wa dubu alitambulishwa kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa Ujerumani huko Gelsenkirchen mwezi Juni 2023, kabla ya mechi ya kirafiki ya timu ya taifa dhidi ya Colombia.

SOMA ZAIDI: EURO 2024 Yaja Na Mpira Wa Roboti, Kugundua Offside Mapema Kuliko VAR

 

2 Comments

  1. Pingback: Huu Hapa Uwanja Wa Fainali UEFA EURO 2024

Leave A Reply


Exit mobile version