Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiondolea klabu ya Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kumlipa aliekua mchezaji wake Gael Bigirimana.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF inasema kuwa Gael alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu ya Yanga kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba na kushind kesi hiyo dhidi ya waajiri wake hao wa zamani.

Yanga baada ya kutekeleza matakwa yote yanayotakikana ya kumlipa mchezaji huyo ndio TFF imewafungulia kufanya usajili wa wachezaji.

Barua kutoka TFF kuhusu kufunguliwa usajili kwa Yanga baada ya kumlipa Gael Bigirimana.

 

Unaweza kuendelea kusoma zaidi kuhusu taarifa zetu za michezo na Makala kwa kugusa hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version