Klabu ya soka ya Yanga imemtambulisha mtaalamu wa kusoma mchezo Mpho Maruping raia wa Afrika Kusini baada ya kutokua na mtaalamu kama huyo tangu kuondoka kwa Khalil Ben Youssef alieungana na kocha Nasredinne Nabi katika kikosi cha ASFAR RABAT.

Mtaalam huyo anaungana na wataalam wengine kikosini hapo kuhakikisha kuwa klabu ya Yanga inafanya vyema haswa kuelekea mech izote walizonazo mbeleni kuanzia michuano ya klabu bingwa barani Afrika lakini pia Ligi kuu Tanzania Bara bila kusahau kombe la shirikisho la Azam.

Mpho amezaliwa tarehe 07/08/1991 nchini Afrika Kusini na aliwahi kucheza mpira kama kiungo wa kati lakini pia akiwa na timu ya taifa ya wanawake katika michuano ya Afrika kwa wanawake ambapo alikua na kazi ambayo imemefanya Yanga wamchukue.

Kwa habari zaidi za michezo na makala mbalimbali unaweza kusoma hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version