Safari ya kikosi cha Yanga ikielekea jijini Lubumbashi iliingia dosari baada ya kukwama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa takribani masaa 12.

Yanga inakwenda Lubumbashi kumalizana na wapinzani wao TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho kiliwasili Uwanja hapo majira ya saa 3:00 kwa safari hiyo ambayo awali ilikuwa ianze saa 5:00 asubuhi ikielekea Lubumbashi kupitia Ndola Zambia.

Hata hivyo muda huo ulipofika walipewa taarifa ya kwamba ndege yao itachelewa na kupangwa kuondoka saa 8:00 mchana lakini pia baadaye ukasogezwa tena mbele na kuambiwa wataondoka saa 11 jioni.

Safari hiyo ikapigwa tena ‘kalenda’ wakiambiwa muda mpya wa kuanza safari hiyo wakitumia Ndege ya Shirika la Tanzania kuwa itakuwa saa 1: 00 usiku lakini muda huu wakapokea tangazo jipya kuwa wataondoka saa 3:00 usiku wakitumia Ndege namba TC 213 sababu ikitajwa kuwa sababu za kiufundi.

Leave A Reply


Exit mobile version