Mechi iliyotarajiwa kuwa nzuri lakini mwenendo wa mwamuzi uliharibu ladha nzima ya mechi! Mwamuzi alikuwa wa kiwango cha chini mno! Kila timu iliona inammudu mwenzie tu na makosa yalikuwa mengi.

Medeama walikuja na mpango wa kujitoa, kufika miguuni na wanafurahia mpira wa kugongana! Wana madhaifu mengi kiufundi na Yanga wangekuwa na matumizi mazuri ya nafasi wangefurahia zaidi.

Yanga kila mchezo wanacheza vyema, wanatengeneza nafasi nyingi ila matumizi yake ni butu mno! Musonda ana papara, Mzize anajigovya govya! Ndio kitu pekee kinachowatafuna mechi baada ya mechi.

Well played Kwadwo Amoako yule jezi namba 4 mchezaji mzuri sana! Mipira yake ya kutenga ni balaa mnoAna uwezo mzuri sana wa kupiga pasi pia na uvumilivu wake mchezoni ni mkubwa sana.

Yule Pacome Zouzoua anajua mpira Anajiamini kutembea na mpira kwenye nyakati usizotarajia. Lile goli na movement ile angekuwa mchezaji mwingine angelazimisha kupasia! Ndiye Man of the Match wangu leo.

Jonathan Sowah achana na goli lake la penati anajua sana kulinda mpira! Juu anaenda, chini anacheza kwa timing nzuri sana. Nilipenda energy yake kwenye kuwania mpira.

Ibrahim Abdullah Hamad ‘Bacca’ na leo tena kwenye ubora wake ule ule kwenye msitari wa safu ya ulinzi Alitembeza mkong’oto vyema tu.

Kipa Felix Kyei ana ‘footwork’ nzuri sana na wenzie wanamwamini sana inapohitajika mazingira ya kujisitiri kwani Mguuni kwake mazungumzo yamo.

Khalid Aucho kwenye mfumo wa mabeki watatu wa kati anajikuta anatembea eneo kubwa peke yake… Anafanya kazi ya ngamia sana kwa sasa.

Yanga wanammiss sana Lomalisa! Kibabage sio mbaya na anaingia kwenye boksi vyema tu ila maamuzi yake akiwa kwenye boksi ni dhaifu mno! Hana uhakika wa anachotaka kufanya!

Yanga leo kuna muda walionekana kama wamechoka kwenye muda ambao Medeama wamechoka!

Kundi hili linazidi kuvurugika! Yanga wameshindwa hii mechi wanapaswa kujilaumu wao wenyewe! Ni experience nzuri na ngumu wanaipata! Kazi imebaki kwenye mikono yao! Soma zaidi

Leave A Reply


Exit mobile version