Anaandika mwana mitandao maarufu Tanzania anayefahamika kama Ujugu Hapa 

Nataka twende taratibu ili tuelewane. Mdogo mdogo mpaka mwisho. Kama unajijua una mihemko, usisome hili andiko, HALIKUHUSU!

Mimi nafahamu sehemu yenye furaha ukileta habari za huzuni watu lazima wakufikirie una vina saba vya uchawi. Kwa sasa Yanga ipo kileleni, kila mwaka inapata mafanikio ya kubeba vikombe, mashabiki wana furaha.

Inapotokea mtu anaisema Yanga kwa namna yoyote ile nje ya furaha waliyonayo, basi huyo mtu anaonekana kama Mchochezi, Mzandiki, na haitakii mema Yanga

Lakini mimi naelewa yote hayo, najitosa ili tukumbushane. Yanga kwa sasa ina furaha, ila ina matatizo na haijitambui. Kuna ‘Utoto mwingi’ unafanyika ndani ya Yanga

Ipo hivi, Tafsiri ya kutojitambua ni kwenda na mambo tofauti na vile inavyotakiwa. — NJE YA UTARATIBU.

Na ukifanya mambo tofauti na inavyotakiwa unakaribisha matatizo

Mimi najaribu kujiuliza je Yanga imekua ni klabu ya WAPARE?

Siongei kwa ubaya kuhusu wapare, ila inafahamika ni watu wanaopenda kesi sana. Sasa hizi kesi ambazo haziishi za Yanga kila msimu zinatokea wapi? Faida yake ni nini? Na anaesababisha ni nani, ili iweje?

Chini ya utawala wa Injinia Hersi, Kila msimu Yanga ina kesi za usajili, kati ya mchezaji na klabu ya Yanga ama Klabu ya Yanga na Klabu nyingine — Kesi kubwa huwa ni PESA ZA USAJILI

Tunarudi pale pale kuwa YANGA INA MATATIZO. Kwanini kila siku kesi ziwe kwao tu?

Naomba niwakumbushe;

> August 2023, Taarifa zilitoka Yanga ilikua na kesi na Gael Bigirimana. Yanga ilipigwa adhabu ya kutosajili mpaka imlipe mchezaji huyo pesa zake. Kesi hiyo ni mule mule tu kwenye matatizo ya pesa za usajili.

> April 12, 2024 Yanga ilifungiwa kufanya usajili kupitia kesi ya mchezaji ambae taarifa ya TFF haikutaka kumtaja jina. Yanga ilitakiwa ikamilishe malipo ya mchezaji huyo.

> April 30, 2024 – Yanga ilikua na kesi na Lazarous Kambole, Fifa wakaingilia kati, Yanga ikashindwa, na ikamlipa Kambole

> August 20, 2024 – Jana zimetoka taarifa Yanga ina kesi na Bechem United. Inatakiwa ilipe zaidi ya milioni 200 kutokana na kukiuka makubaliano wakati wanamsajili Okrah

> Yanga ilikua na kesi na Hafiz Konkoni. Kesi ya pesa za usajili. Nani hakumbuki hili?

> Yanga ilikua na kesi na Morrison, walivutana mashati sana, ila Yanga ikashindwa ile kesi

Hizi kesi zote, hakuna kesi hata moja ambayo Yanga ameshinda. Je hii inatupa picha gani?

> Moja, Inawezekana kitengo cha Sheria ndani ya Yanga ( Department of compliance) ina udhaifu, au inapungukiwa uzoefu wa kudeal na kesi za kimkataba za wachezaji

> Mbili, Inawezekana ndani ya Yanga kuna ‘Mtu’ anaichomesha Yanga kupata hizi kesi ili
‘Labda’ ajitengenezee mazingira ya kuipiga Yanga pesa

> Tatu, Inawezekana ndani ya Yanga usajili unafanywa kwa mihemko, na kupelekea kushindwa kufanya makubaliano vizuri ya kimkataba na wachezaji wanaosajiliwa

> Nne, Inawezekana Yanga inahitaji kuongezewa nguvu na wanasheria wenye uzoefu na mikataba ya wachezaji hasa wa kimataifa. Kwa kuwa ukiangalia kesi zote zilizotokea, hakuna kesi hata moja iliyomhusu mchezaji wa ndani ( Local Player)

> Tano, Juzi tu kulikua na kesi ya Magoma, inayoihusisha Yanga kupitia baraza la wadhamini. Nadhani ndio kesi pekee Yanga amepata ushindi, japo hisia zangu zinaniambia, huko mbeleni hii kesi itakuja kufufuka tena

Mtazamo wangu ni kuwa YANGA INA MATATIZO.

YANGA HAIJITAMBUI.

Laiti kama Yanga ingekua inajitambua, hizi kesi zisingekua zinajirudia.

Najua kwa sasa Yanga ina furaha, hakuna anaetaka kusikia hizi habari. Ila ipo siku isiyo na jina, kwa ninavyoijua Yanga na watu wake, watakuja kufukua haya makaburi ya hizi kesi

Sasa ni muhimu Yanga ijirekebishe kabla JUA HALIJAZAMA.

Ila kama hamtaki kunisikiliza, endeleeni kujificha kwenye kivuli cha furaha, na kuendekeza hizi kesi.

Bwana Yesu Asifiwe.
#UJUGUHAPA

SOMA PIA: Kwa Maboresho Haya Wadhamini Wa Ligi Kuu Mmetisha

22 Comments

  1. Baisar s Mjobwe on

    UJUGU UMEONGEA POINT SANA,SEMA KITU KIMOJA KIBAYA SANA ULICHOKITUMIA KWAMBA YANGA HAIJITAMBUI,NAFIKIRI UKASO.E VIZURI MAANA YA NENO KUJITAMBUA
    MAKOSA YANAYOTOKEA NI KWELI LAKINI HATA WW UMEANDIKA KWA MIHEMKO SANA

  2. Siku zote mti wenye matunda hupigwa mawe .mm ninachokijua ni kwamba haya mambo ipo siku yatakaa sawa na matatizo siku zote hayaepukiki 1113.
    Naiombea dua management ya young Africa iendelee kusimama imara ili mwisho wa siku Kila kitu kitakaa sawa.

    • Kashinje Mussa on

      Safii sana tunaiombea pia kila kitu huwa kina mwisho na huwezi pata mafanikio bila changa moto ndogo ndogo naimani yanga African itakuwa itakuwa imala tu kwene mambo kama hayo

  3. Huyu aliyeandika nadhani anaweza kuwa na hoja ila akatumia maneno ya kimihemuko kuiwasilisha hvyo kuonekana yeye ndo hajitambui

  4. Upo sahihi brother lkn unapokosoa tumia lugha nzuri iyo ya hatujitambui siyo nzuri, mimi nakubaliana na wewe kwenye kitengo cha sheria cha klabu yetu kina madhaifu sana,ngoja tujifanye hatuoni tufurahi muda wa kuteseka ukifika tutateseka.

  5. Chris Mlangwa on

    Mr UJUGU HAPA upo sahihi , mathalani hata kwa kutumia neno HAWAJITAMBUI , kwa maana kwao waona ni kawaida kuwa na mfululizo wa kesi , la hasha ! walipaswa watatue mapema lakini kwakuwa zinaendelea basi nadiriki kusema HAWAJITAMBUI KABISA 📌

  6. Yan unachoongea hakijawahi kuepukika kwa Tim yoyote ile hapa dunian kila club huwa na matatizo ya kiusajili lakin kwa ulivyo iongelea yanga naona kabisa yanga inakuumiza kichwa kwa makali yake

  7. Pingback: Takwimu Na Rekodi Za CBE SA Wapinzani Wa Yanga Ligi Ya Mabingwa Afrika

  8. Kama wewe unajitambua kawe mtu wa sheria wa yanga ila naona wew ndo hujitambui na hujui sheria kila tu ana haki ya kushitaki na kushitakiwa ,? Na pia inaonesha dhahiliii hujui kama iyo timu yako ambayo hujaitaja jina kam na yenyewe huwa inashitakiwa vile vile #JITAMBUE NDO USEME

Leave A Reply


Exit mobile version