Ukiutazama mchezo wa Yanga dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ni wazi kuwa kwa namna ambavyo mchezo ulivyokua na jinsi ambavyo Yanga walikua wanacheza ni wazi kuwa walikua wanauhitaji zaidi ushindi katika mchezo huu ili kuweza kushusha presha kwa mashabiki baada ya sare dhidi ya Kagera Sugar.Goli la kwake Mudathir Yahya Abbas likiwapa Yanga alama 3 katika uwanja ambao amekua kisoka kuanzia akademi ya soka mpaka kucheza timu kubwa ya Azam Fc.

Licha ya nafasi nyingi ambazo walizitengeneza na kuzikosa lakini hawakukata tamaa na kuonesha kuwa walikua na uhitaji mkubwa sana katika mchezo huu.

Ukiwatazama namna ambavyo Dodoma walikua wanacheza walikuja na muundo mzuri wa kuzuia na kuwaheshimu wananchi  huku wakicheza kwa kushtukiza.

Unaweza kusifu uwezo wa makocha wote lakini ni wazi lazima umsifie kocha wa klabu ya Yanga kwani Mabadiliko ambayo ameyafanya yameweza kumlipa na kumfanya aondoke na alama 3 katika dimba la Chamazi.

Siku zote haijawahi kuwa rahisi mchezo unaowakutanisha Dodoma na Yanga licha ya kuwa wananchi wao wanaongoza kwa takwimu nzuri zaidi mbele ya walima zabibu wa Dodoma.

Ushindi wa leo unawapa nafasi ya kupumua wachezaji wa Yanga na kushusha presha ya kupambania ubingwa wa ligi kuu kutokana na upinzani mkubwa uliopo kutoka kwa Azam Fc na Simba Sc.

SOMA ZAIDI: Ligi Kuu Imerejea Marefa Kuweni Na Msimamo

Leave A Reply


Exit mobile version