Wakati Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said anamchukua Ibrahim Bacca kutoka katika klabu ya KMKM ya Zanzibar bila shaka hakuna aliyemuelewa anafanya nini na kwanini kaamua hivyo kwani bila shaka mashabiki wa soka na wanachama wa Yanga wameshazoea baadhi ya majina makubwa pekee yakiwa yanasajiliwa katika kikosi chao huku wakiwa na Imani ya kuwa atafanya vyema kwenye kikosi chao.

Mwaka jana klabu ya Yanga waliona thamani ya Ibrahim Bacca na kumuongezea mkataba mrefu zaidi wa hadi mwaka 2027 ili aendelee kuitumikia klabu hiyo yenye makao yake makuu katika mitaa ya Twiga na Jangwani baada ya kazi kubwa aliyoifanya katika mwaka mmoja na nusu ambao aliwatumikia wananchi.

Kwa sasa ndio tunakuja na kuamini kuwa huyu ni moja kati ya mabeki bora kutoka Zanzibar waliowahi kuitumikia klabu ya Yanga kutokana na kiwango bora ambacho ameendelea kukionesha katika kikosi cha Yanga lakini pia na timu ya Taifa ya Tanzania.

Yanga wanafahamu kabisa kuwa kupitia michuano ya kimataifa ambayo walikua wanashiriki huku Bacca akiwa miongoni mwa wale wanaokitumikia kikosi chao bila shaka kabisa kuna klabu zilikua zinamtazama katika jicho la kibiashara zaidi ukitazama kuanzia michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambayo walifika fainali mpaka michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambayo wako mpaka sasa.

Katika michuano ya mataifa barani Afrika ambayo mara nyingi maskauti wa timu mbalimbali barani Ulaya na mawakala wa wachezaji huitumia kama njia ya kutafuta vipaji vipya na kutengeneza pesa ila kwa Ibrahim Bacca ni wazi lazima waende mezani na kujadiliana thamani ya mchezaji na kumuuza na kufaidika katika biashara ya mpira zaidi.

Licha ya kuwa Tanzania haijafika mbali katika AFCON il ani muda sahihi wa Ibrahim Bacca kuongeza nguvu zaidi katika mazoezi na kujituma kwani kwa kiwango alichonacho na uwezo wake wa kupambana ni aina ya mabeki ambao wanahitajika katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya AFCON Hatua Ya 16 Bora

1 Comment

  1. Pingback: TFF Ni Wakati Wa Kuwafungulia Fursa Nje Makocha Wazawa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version