Kama ni mchezo uliongoza kuteka hisia za watu ndani ya muda mfupi wa kukutana kwa timu hizi mbili basi ni mchezo huu wa Leo timu zote mbili yaani Yanga na Ihefu zina matokeo yanayofanana kwenye michezo yao ya mwisho kwani wamecheza jumla ya michezo 4 huku kila mmoja akishinda michezo miwili na michezo yote kila timu ilipatia ushindi kwenye uwanja wake wa Nyumbani.

Mchezo wa Yanga SC na Ihefu FC ni mchezo ambao umekuwa ukiteka hisia ya kulipa kisasi pale wanapokutana huu ni msimu wa pili sasa, takwimu zao kwa ujumla walianza kukutana kwenye michezo ya Ligi kuu kwa mara ya kwanza 2020 ambapo mpaka sasa wameshacheza jumla ya michezo mitano huku Yanga SC akiibuka na ushindi kwenye michezo 3 na Ihefu FC akishinda michezo 2 tena yote akiwa kwenye uwanja wake wa Nyumbani.

Uzuri ni kuwa kila mchezo utakaowakutanisha baina yao umekuwa ukizalisha goli na hakuna mchezo ambao timu mojawapo imeshinda kwa magoli mengi ni siyo zaidi ya magoli matatu na Mara ya mwisho timu moja kumfunga mwenzake goli nyingi kwenye mchezo mmoja ni 2020/2021 Yanga SC akiibuka na ushindi wa 3-0 ugenini kwa magoli Ya Deus Kaseke, Yacouba Sogne na Feisal Abdallah “Feitoto”

Wachezaji wanaongoza kufunga magoli kwenye mchezo unaowakutanisha ni Feisal Salum akiwa na magoli matatu ambaye kwa sasa siyo sehemu ya kikosi hicho, akifatiwa na Lenny Kisu akiwa na magoli mawili na mpaka sasa bado anahitumikia Ihefu FC hivyo ana nafasi ya kuongeza goli. Michezo yao 5 ya mwisho ya Ligi kuu ya NBC Ihefu FC ameshinda 3 akitoa sare 1 na kufungwa mmoja huku Yanga SC akishinda michezo mitano akifunga magoli 11 na akiruhusu magoli 3 tu.

Ihefu FC hawakuanza vizuri ila kwenye michezo yao ya hivi karibuni wamekuwa na kiwango bora sana kuanza namna wanacheza kiwanjani, wanavyotengeneza nafasi na wanavyolinda, chini ya Mecky Mexime wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-4-2 na wakati mwingine 4-3-3 ambapo Elvis Rupia amekuwa akisimama eneo la juu na nyuma yake akiwa Marouf Tchakei huku wakati mwingine Tchakei amekuwa akitokea pembeni kuingia ndani na ndiyo sababu ya kufunga magoli mengi akiwa mzuri kumalizia mipira ya pili inayotua “second ball”.

Moja ya tatizo kubwa kwa Ihefu FC licha ya kuwa wazuri kutumia nafasi chache wanazopata lakini wamekuwa wakiruhusu zaidi magoli jambo ambalo wasipobadilika kwenye huu dhidi Ya Yanga SC basi itakuwa rahisi kwao kupoteza mchezo na kudondosha alama.

Upande wa Yanga SC wamekuwa wakitumia zaidi 4-2-3-1 na wamekuwa wakiutekeleza vizuri ambapo eneo la mwisho amekuwa akisimama zaidi Clement Mzize huku Pacome Zouzoua, Max Nzengeli na Stephane Aziz Ki wakitokea zaidi pembeni mwa uwanja wakiingia ndani na Mara nyingi ni Pacome na Max huku Aziz Ki akitokea katikati mwa uwanja wakibadilishana nafasi, uwepo wa Mudathiri Yahya umekuwa ukiwapa ufanisi zaidi kwenye upatikanaji wa magoli kwani amekuwa mzuri sana kwenye mipira ya pili kwenye 18 ya mpinzani.

Licha ya kufunga magoli mengi ila pia wamekuwa na safu nzuri Ya ulinzi na imekuwa ngumu kuwafunga kwani wamekuwa wakikaba kwa kuanza kupress kuanzia eneo la juu (kupitia washambuliaji wao) na Mzize amekuwa akifanya vyema sana hiyo kazi.

Mchezo huu utakuwa na vita kubwa sana kwenye maeneo yote mawili Ya ushambuliaji kwa timu zote mbili pamoja na eneo la kati la ukabaji, hata hivyo kukosekana kwa Khalid Aucho linaweza kuwa pengo kwa Yanga SC kwani amekuwa mzuri sana kuiongoza timu ikiwa uwanjani iende kwa kasi au taratibu hata hivyo amekuwa mzuri kuanzisha mashambulizi kutokea chini wakiwa na “Pattern” nzuri na Mudathiri Yahya na wakati mwingine imekuwa ngumu kuwafanyia “Press” akiwepo uwanjani.

Ni mchezo ambao tutashuhudia kandanda safi kwa pande zote mbili kwani timu zote zimekuwa zikiweka mpira chini na kuanzisha mashambulizi kuanzia chini (eneo la ulinzi) hususa kupitia kwenye beki zao za pembeni kulia na kushoto na wamefanikiwa kwenye ilo. kumbuka kuwa kwenye michezo 5 ya mwisho ya Ligi kuu ya NBC Yanga SC imefanikiwa kufunga magoli 11 na kuruhusu magoli matatu tu huku kwa upande wa Ihefu FC wamefanikiwa kufunga magoli 8 na kuruhusu magoli sita jambo ambalo kuna uwezekano kila kitu ikapata goli kwenye mchezo huo.

SOMA ZAIDI: Simba Wangeanza Na Huyu Anayeleta Wachezaji

1 Comment

  1. Pingback: Alichofanya Mwigulu Kwa Ihefu Ni Kawaida Tu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version