Matokeo yao ya mwisho walipokutana kwenye raundi ya kwanza ni Yanga SC aliibuka na ushindi wa goli 3-0 magoli yakifungwa na Pacome Zouzoua, Max Nzengeli na Aziz Ki. Mchezo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwenye mji wa Mwanza.

Timu hizo zimefanikiwa kukutana mara tanò kuanzia msimu wa 2021/2022 na katika kukutana kwao klabu Ya Yanga SC amefanikiwa kushinda michezo yote mitano ambapo wakiwa Nyumbani amefanikiwa kushinda michezo 2 na ugenini wakiibuka na ushindi michezo 3 huku wakifunga magoli tisa (9) na wakifanikiwa kufungwa goli moja tu. Timu hizo zimecheza michezo mitatu mfululizo na Yanga SC kuibuka na matokeo ya goli 1-0 pia wamecheza michezo miwili mfululizo na kushinda kwa goli 3.

Mpaka sasa Mchezaji anayeongoza kufunga magoli mengi timu hizo zikikutana ni Jesus Ducapel Moloko ambaye kwenye michezo mitano amefanikiwa kufunga magoli 2 mengi kuliko Mchezaji yeyote yule. Michezo yao mitano Ya mwisho Ya Ligi kuu ya NBC Geita Gold FC amefanikiwa kuibuka na ushindi mchezo mmoja, akipata Sare michezo 2 na akipoteza michezo 2 huku akiruhusu magoli 6 na akifanikiwa kufunga magoli matatu (3) na kukusanya jumla Ya alama 5 tu.

Huku kwa upande wa Yanga SC ndani ya michezo mitano Ya mwisho Ya Ligi kuu ya NBC amefanikiwa kushinda michezo yote mitano akifunga magoli 15 huku akifungwa magoli matatu tu na kukusanya jumla Ya alama 15.

Ubora wa Yanga SC kwa sasa ni mkubwa sana na hiyo imetokana muunganiko uliyopo kwenye kikosi chao, wakitumia zaidi mfumo wa 4-2-3-1 wakiwa na viungo wengi washambuliaji Pacome, Aziz Ki na Max Nzengeli. Ubora wao Upo wapi ? eneo Lao la Kiungo ni muhimu mkubwa sana kwao, moja uwepo wa kiungo wao mkabaji Khalid Aucho (majeruhi kwa sasa) imekuwa ndiyo silaha yao kubwa akiamua namna ambavyo watacheza kwa haraka au taratibu, pili uwepo wa Pacome, Aziz Ki na Max Nzengeli umekuwa ni hatari sana kwa mpinzani hususa kwenye “transition” wana uwezo wa kutumia kasi au pasi fupi na ndefu pia, tatu ni mabeki wao wa pembeni uwepo wa Yao Attohoula upande wa kulia na Nickson Kibabage pamoja na Joyce Lomalisa upande wa kushoto wamekuwa wakisaidia mashambulizi na wamekuwa rahisi kurudi na kutekeleza majukumu yao mama ya kukaba.

Udhaifu wao huko kuelekea mchezo huo ? Moja kabisa ni kukosekana kwa Kiungo wao Khalid Aucho ambaye amekuwa akiweka muhimili mkubwa sana hususa kwenye kukaba pale timu inapokuwa haimiliki mpira jambo ambalo kwa sasa haitekelezwi ipasavyo na Salum Abubakar. Nini wafanye Geita Gold kutumia udhaifu huo ? Ni kutumia miaya inayoachwa na kiungo Salum Abubakar na Mudathiri Yahya hususa pale wanapojenga shambulizi na kuwa kwenye nusu Ya mpinzani.

Geita gold wamekuwa wakitumia 4-4-2 wakimtumia Yusuph Mhilu na Valentino Mashaka kwenye eneo Lao la mwisho huku Samwel Onditi na Geofrey Julius wakitumika zaidi kama viungo wakabaji na moja na tegemezi kubwa kwao ni uwepo wa golikipa wao Constantino amekuwa na kiwango bora sana kilichowafanya kuwapa alama muhimu kwenye baadhi Ya michezo. Huku uwepo wa mshambuliaji wao Tariq Seif Kiakala amekuwa akifunga magoli muhimu sana kwenye kikosi hicho.

Udhaifu wao uko wapi ? Moja Ya udhaifu wao mkubwa ni kuacha nafasi kubwa hususa wakiwa wanashambulia na zaidi wamekuwa wakishindwa kumalizia “transition” vizuri na imetokana na kupoteza mpira husua pale wakikutana na timu inayoamua kukabia kwa juu.

Nini wafanye ili waweze kuwa na mchezo mzuri au kuondoka na alama kwenye mchezo huo ? Jambo kubwa kabisa ni kukubali kukimbia eneo kubwa la uwanja na kukubali kwenye Low block huku wakiwa na matumizi mazuri Ya “Caunter attack” na kutumia nafasi watakazopata kwa usahihi.

SOMA ZAIDI: FIFA SERIES 2024 Ni Michuano Gani? Na Inafanyikaje? 

Leave A Reply


Exit mobile version