Simba itashuka dimbani leo kuanzia saa tisa alasiri kwa saa za Tanzania kwenye Uwanja wa Stade Mohamed V mjini Casablanca, Morocco. Tayari wachezaji wa Simba wamewasili Casablanca kabla ya pambano lao

Yanga itashuka dimbani Jumapili kuwakaribisha Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mechi hiyo itaanza saa 7 mchana.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemteua mwamuzi wa Chad Alhadi Allaou Mahamat kuchezesha mchezo wa robo fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC ya Tanzania na Wydad Club Athletic ya Morocco.

Simba itashuka dimbani leo kuanzia saa tisa alasiri kwa saa za Tanzania kwenye Uwanja wa Stade Mohamed V mjini Casablanca, Morocco. Tayari wachezaji wa Simba wamewasili Casablanca kabla ya pambano lao.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, Mahamat atasaidiwa na Elvis Guy Noupue Nguegoue kutoka Cameroon na Issa Yaya, pia kutoka Chad huku afisa wa nne atakuwa Mahmood Ali Mahmood Ismail kutoka Sudan.

Simba ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na inahitaji sare yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Hata hivyo, Simba itakosa huduma ya wachezaji wake watatu, Aishi Manula, kipa chaguo la kwanza ambaye sasa anauguza jeraha lake, Augustine Okrah na Mohamed Ouattara. Kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo almaarufu Robertinho, alisema wataenda kuthibitisha thamani yao katika pambano hilo licha ya kukabiliwa na kibarua kigumu.

Alisema wachezaji wake wapo katika hali nzuri na wako tayari kufanya vyema katika mechi hiyo.

Wakati huohuo, mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa Yanga na Rivers United, utachezeshwa na waamuzi wa Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, Redouane Jiyed atakuwa katikati ya uwanja katika pambano hilo gumu ambalo Yanga inahitaji sare yoyote ili kuweka historia ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Yanga ilishinda 2-0 ugenini na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Jiyed atasaidiwa na Lahcen Azgaou na Mostafa Akarkad huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Jalal Jayed, pia kutoka Morocco.

Wachezaji wa Yanga wameanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 7 mchana Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Licha ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, alisema wanaichukulia kwa uzito mchezo huo na wanalenga ushindi ili kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya kifahari.

Yanga ilishinda 2-0 ugenini na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Jiyed atasaidiwa na Lahcen Azgaou na Mostafa Akarkad huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Jalal Jayed, pia kutoka Morocco.

Leave A Reply


Exit mobile version