Kumekua na takwimu nyingi sana mtandaoni pamoja na maandiko kadha wa kadha haswa zikizihusisha klabu kubwa mbili hizi kubwa kuhusiana na ubora wao kimataifa na hii imekuja baada ya ushindi wa kishindo walioupata mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga.
Kumbuka kuwa wananchi wamepata ushindi dhidi ya mabingwa mara 4 mfululizo wa ligi kuu ya Algeria klabu ya CR Belouizdad ambapo sasa kumeibuka hali ya kuweweseka kwa baadhi ya wachambuzi lakini pia na mashabiki wa klabu ya Simba hali inayoonekana kuwa vivyo hivyo mpaka kwa meneja Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally.
Kutokana na ushindi wa Yanga, zimeanza kuibuliwa rank za mchongo za CAF, mara zinaibuka hoja Simba sc ndio timu kubwa pekee Afrika, zinaletwa historia za mwaka 1977 kwamba waliwahi kufika nusu fainali klabu bingwa Afrika lakini jambo zaidi ambalo limenisikitisha ni kuhusu kuwa Mo Dewji ndie aliesababisha mafanikio ya Yanga hapa mnawakosea heshima Yanga pamoja na mdhamini wa klabu hiyo GSM, lakini pia wakitajwa Horoya walivyofungwa goli saba.
Yaani yote haya kisa Yanga katinga robo fainali? Kwamba kile kichaka walichokua wamejificha ni wazi kuwa sasa kimefikiwa basi yanaibuka mapya kila siku? nashindwa hata kushangaa kwa kiwango hiki kidogo kinachooneshwa cha kufikiri kuhusu soka la nchi yetu.
Yaani mashabiki wa Yanga sc hawatakiwi kushangilia matokeo na mafanikio ya timu yao sababu wekundu wa msimbazi walishawahi kufanya?. Tukisema hii timu ni kituko cha taifa wanatukana.
Ukiangalia mpaka sasa Simba ina point 39 huku Yanga ikiwa na point 31 kama ni watu wa kustuka basi walipaswa kuona kuwa hii ni wakeup call kwenu Simba kwasababu gap ya point ilikuwa kubwa sana yaani kutoka 0.5 hadi 31 kwa misimu miwili tu mfululizo. Kama Simba ikiachwa hatua moja tu na Yanga inamaana gap ya point 5 zitapungua. Na kama Simba akiachwa hatua mbili ina maana Yanga atajipatia point 10 ambazo ukitoa 8 za Simba inamaana Yanga itakuwa juu ya Simba kwa pont 2.
Mna kazi ya kufanya ili kujitetea kwenye hiko kichaka cha ranking kwasababu soon nacho kinaenda kufyekwa. Mkizubaa basi msimu huu huu kinafyekwa kama kilivyofyekwa kichaka cha robo fainali ya CAFCL.
SOMA ZAIDI: Ahmed Ally Uko Sahihi Ila Wakati Uliotoa Kauli Yako Sio Sahihi
1 Comment
Pingback: Hawa Makomando Simba Na Yanga Huwa Wanalinda Nini? - Kijiweni