Wakati Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2022/23 ikifikia mwisho Ijumaa ya Juni 9, 2023, Mdhamini Mkuu wa ligi hiyo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kombe jipya la ligi kuu lililoboreshwa.

Kombe hilo limezinduliwa Juni 7, 2023 jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na litakabidhiwa kwa bingwa mtetezi, timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam ambayo wamekwisha tangazwa washindi.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa benki hiyo, Godwin Semunyu amesema NBC ikiwa kama mdhamini mkuu wa ligi imeboresha kombe kutokana na maoni ya wadau mbalimbali wa soka.

“Kwa sasa ligi yetu ni ya tano kwa ubora Afrika na hii ni hatua kubwa na nzuri kwa soka letu. Leo tumezindua kombe lililoboreshwa ikiwa pia ni sehemu ya kuongeza thamani kwa ligi yetu,” amesema.

“Benki itaendelea kutoa mchango wake katika kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchni kwa kuwa inatambua umuhimu na mchango wa michezo kwa maendeleo,” amesema
Naye Mkurugenzi wa Fedha wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela amesema udhamini wao umekuwa wenye tija kubwa kwa ligi na ni mdau mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini.

Leave A Reply


Exit mobile version