Kuelekea mchezo wa hapo baadae Medeama dhidi ya Yanga, nauona mchezo ambao Yanga watataka kuutumia ili kurejesha matumaini yao. Medeama tayari wana alama 3 huku Yanga mwenye alama mbili atahitaji ushindi wake wa kwanza, na ili kupata ushindi wa kwanza lazima ashambulie zaidi ili kufunga mabao.

Sasa changamoto inakuja kwa aina ya uchezaji wanaotumia kasi zaidi kupitia mawinga wao, na hapo Yanga wanatakiwa kuwa makini zaidi kupitia counter attacks pale wanashambulia.

Na ili kuwa makini zaidi wanatakiwa kuwa na rest defense bora pale wanashambulia kutafuta ushindi, maana Medeama watatumia zaidi counter attacks pale watakapopora mipira kwa yanga.

Faida ya Yanga ni ubora wa kikosi chao kwa sasa,kinaundwa na wachezaji wenye ubora na uzoefu pia kwahiyo wapo na nafasi ya kushinda kama watakuwa bora na imara kwenye kutengeneza na kutumia nafasi.

Mchezo wa leo umebeba taswira nzima ya Yanga kwenye kundi, kwa sababu ushindi kwao utafufua matumaini lakini matokeo ya kufungwa au sare yanaweza kukatisha tamaa.

Miongoni mwa washambuliaji hatari wa kikosi cha Medeama kutoka nchini Ghana.

Note: Medeama wanaelewa nini yanga wanahitaji kwahiyo wataingia wakiwa hawana shinikizo kubwa tofauti na Yanga na hilo linaweza kuwa faida au hasara kwa Yanga.

Faida kutokana na shinikizo la Yanga ni kucheza kwa ubora mkubwa na kutumia nafasi lakini hasara ni pale watakapopoteza utulivu kutokana na shinikizo hilo.

Katika mechi 6 ambazo timu zote zimecheza, Medeama yeye ameshinda mechi 3 na kusare mechi 1 na kupoteza mechi 2 wakati wananchi wao ( Yanga) katika mechi 6 wameshinda mechi 4 sare mechi 1 na kufungwa mechi 1.

Msimamo wa kundi lao ambalo kuna timu kama AL AHLY , CR BELOUIZDAD na MEDEAMA klabu ya Yanga wao wana alama 1 pekee ambayo ilikua ni sare dhidi ya Al Ahly huku wengine wote wakiwa wameshinda mechi zao za kwanza huku Yanga akipoteza kwa mabao matatu mbele ya CR Belouizdad ya nchini Algeria.

Mchezo wa leo utapigwa majira ya saa 1 kamili za jioni . Vipengele vya tuzo za CAF hivi hapa 

Leave A Reply


Exit mobile version