Moja ya eneo ambalo kikosi cha Yanga SC kimekuwa imara zaidi basi ni eneo lake la katikati uwepo wa viungo wakabaji wazuri wenye kasi na nguvu pia kama Khalid Aucho na Mudathiri Yahya imefanya kuwa ngumu sana kupitika, hata hivyo wamekuwa bora kwe ye kiungo cha ushambuliaji zaidi eneo la katikati, uwepo wa kiungo Pacome Zouzoua, Max Nzengeli, Abubakari Salum pamoja na Stephane Azi Ki akiwa juu zaidi.
Uimara huo umeifanya kuwa klabu inayoongoza kwenye Ligi kuu Tanzania bara wakiwa wanawachezaji vinara kwenye kufunga magoli ambapo kwenye 10 bora ya wafungaji wana wachezaji wanne wenye magoli mengi huku wakiwa na wachezaji watatu waliyona (Assist) nyingi, kitendo ambacho kimefanya kuwa moja ya timu tishio nchini na hata kimataifa pia.
Eneo ambalo limekuwa likiibeba zaidi klabu hiyo ni eneo lao la kiungo kwa ujumla kuanzia kukaba na hata ushambuliajia pia, huku moja ya mchezaji ambaye amekuwa bora zaidi na muhimu kikosini akiwa ni Pacome Zouzoua akiwa ndiye mchezaji mwenye hatari zaidi kikosini.
Kwanini Pacome Zouzoua ni mchezaji hatari kikosini ? Moja ya sababu kubwa ni uwezo wake mkubwa wa kuificha mali (mpira) akiwa bora kwenye kupunguza wachezaji wa timu pinzani lakini jambo la pili ni kurudi kusaidia kukaba, kwani pale timu ishambuliwapo anaweza saidia kukaba pia kwa kushuka chini zaidi kuchukua mipira.
Ikiwa ni kuelekea mchezo wao wa “Derby” mchezaji huyo ameshakosekana kwenye michezo mitatu na zaidi bila uwepo wake ila bado pengo lake kikosini linaonekana, sasa ikiwa ni kuelekea mchezo wa “Derby” kuna umuhimu gani mchezaji huyo kuwepo au athari gani akikosekana ?.
Kwanza kabisa hakuna anayebisha ubora wa kiungo huyo kwenye Ligi msimu huu, hivyo kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC pengo lake haliwezi kukosekana japokuwa kikosi kimekuwa kikimkosa kwenye michezo kadhaa ila kimepata ushindi na kuonyesha mchezo mzuri, kwanini mchezo huo ni muhimu, moja kabisa ni ubora wake wa kushambulia akitokea pembeni na katikati pia huku pia akiwa na uwezo wa kushuka chini kuchukua mpira na hata mchezo wao wa mwisho walipokutana alionyesha ubora huo akishuka chini kuchukua mpira kushoto, kulia na katikati pia na kuanzisha mashambulizi na wakati mwingine kumalizia pia.
Je, ikitokea mchezaji huyo hajacheza kuna athari gani kwa timu yake ? Kwa namna Yanga SC inacheza ni ngumu kuona pengo lake kwa sasa ila kuna kasi kidogo ya kushambulia imepungua na hata namna ya uchezaji akiwepo na asipokuwepo inaonekana, Pacome Zouzoua amekuwa bora na ameongeza utulivu sana akifika eneo la mwisho la mpinzani yaani kwenye “box” ya mpinzani na hata ukikumbuka mchezo dhidi ya CR Belouzdad alivyokuwa anacheza hilo linadhihirika.
Hivyo ni dhahiri kuwa ikitokea amecheza mchezo huo basi Yanga SC watanufaika zaidi naye kwenye eneo la mbele zaidi kuliko nyuma na kuifanya safu ya kiungo ya kikosi hicho kuwa hatari zaidi kwenye mchezo huo.
Ila pia kwa namna wanavyocheza sasa hata ikitokea hatokuwa sehemu ya mchezo huo bado apatakuwa na athari yoyote ile kwenye kikosi hicho na hiyo imesababishwa na ubora na uwepo wa wachezaji wengine ambao wanaweza kutumika kwa namna nyingine kimbinu au mfumo tofauti nje ya yeye, na hiyo inaonyesha kuwa kocha Miguel Gamondi amejitahidi kuunda kikosi chake kucheza hata kama kinamkosa mchezaji muhimu kikosini.
SOMA ZAIDI: Yanga Ya Gamondi Inamchanganyia Mafaili Benchikha ?
4 Comments
Simba nitim inayo jiamin
Ni kweli kwa jinsi yanga anavocheza mpira ni ngumu kuona pengo lake ila ingependeza kesho angekuwepo ila mechi iwe ya ushindani zaidi.
Katika Hali Ya Ushabiki Hii Mechi Inaweza Kuonekana Ngumu Kwa Upande Mmoja Ama Kuonekana Nyepesi Kwa Upande Mwingine Ila Hii Mechi Ni Ngumu Sana Tutarajie Matokeo Tofauti Na Fikra Zetu
Pingback: Simba Wanatakiwa Kufanya Haya, Ili Kurejea Kwenye Ubora - Kijiweni