Moja ya mchezo mkubwa sana nchini mchezo ambao umekuwa ukiteka hisia kali za watu wengi huku ukiwa unafatiliwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania, Mchezo huu maarufu nchini kama “Derby ya Kariakoo” ambao daima umekuwa ukiwakutanisha Simba SC pamoja na Yanga SC kwa nyakati tofauti.

Siku zote Yanga SC na Simba SC wakicheza umekuwa mchezo mzuri sana na vita zao mara nyingi ufanyika ndani na nje ya uwanja, ukizungumzia nje ya uwanja ni mbwembwe pamoja na hisia na tambo za mashabiki mbalimbali wa soka, na unapozungumzia ndani ya uwanja ni wachezaji wa timu zote kucheza kiwanjani na kushuhudia vita ya mbinu, mifumo na ufundi wa Wachezaji na makocha kwa pande zote mbili.

Takwimu na Kumbukumbu za timu hizi kwenye michezo yote misimu yao 7 ya mwisho kwenye Ligi kuu ya Tanzania kurudi nyuma kuanzia msimu huu imekuwa migumu sana kwa timu zote mbili ambapo ushindi kwa timu zote mbili haupishani sana kwani Yanga SC amefanikiwa kushinda jumla ya michezo hiyo ameshinda 2 huku akiwa na Sare 4, ambapo kinyume chake ni kuwa Simba SC amefanikiwa kushinda mchezo mmoja (1) na kutoka sare 4 ikiwa ni utofauti wa ushindi kwa mchezo mmoja pekee.

Hata hivyo mpaka sasa mchezaji anayeongoza kufunga magoli kwenye michezo hiyo 7 ya mwisho ya “Derby” walipokutana ni Stephane Aziz Ki wa Yanga SC pamoja na Kibu Denis wa Simba SC ambao wote wana magoli mawili na uzuri ni kuwa wana uwezo wa kuongeza magoli hayo kwani bado ni sehemu ya vikosi vya timu zote mbili.

Hata hivyo nje ya takwimu na kumbukumbu hizo kwa ujumla ndani ya michezo 7, kwenye upande wa michezo mitano ya mwisho ya Ligi kuu ya NBC na michuano mingine ni kuwa Simba SC wamepoteza michezo miwili, wakitoa sare moja pamoja na kushinda michezo miwili na kwa uoande wa Yanga SC amepoteza mchezo mmoja na kutoa sare 2 na kushinda michezo 2, kwenye kufunga magoli Yanga SC amefunga magoli 5 akiruhusu 1 na uoande wa Simba SC amefunga magoli 6 huku akiruhusu magoli 5 tofauti ya goli moja la kufunga na kufungwa.

Ukija kwenye upande wa uchezaji kiwanjani Yanga SC amekuwa bora zaidi kuliko Simba SC msimu huu, kwanini ? Timu yao imekuwa na muunganiko mzuri kuanzia nyuma mpaka eneo la mwisho la ushambuliaji wakiwa na uwiano mzuri wa kukaba na kushambulia pia, ila kwa upande wa Simba SC wamekuwa vizuri kutoka nyuma kwenda mbele changamoto kubwa ni eneo lao la kati kwenye kukaba wamekuwa wakiruhusu nafasi kwa mpinzani kuwashambulia kwa kukosa muunganiko mzuri wa kukaba hususa eneo la kati.

Timu zote zimekuwa zimekuwa zikitumia zaidi eneo lao la kati ambapo ndiyo imekuwa eneo lao mama zaidi kuanzia kukaba na kushambulia. Tofauti yao hiko wapi ? Moja ni eneo la kiungo, upande wa Simba SC wamekuwa wazuri eneo la ushambuliaji ila changamoto ipo kwenye kiungo ukabaji wameshindwa kuwa na kiungo mkabaji ambaye atailinda vizuri eneo lao la beki jambo ambalo linafanya wanapitika kirahisi tofauti na Yanga SC ambao wanakiungo cha ukabaji kizuri kuliko Simba SC.

Eneo hatari zaidi kwenye mchezo wa leo ni kiungo hususa kiungo cha ushambuliaji kwa pande zote mbili wamekuwa vizuri kwenye kutengeneza nafasi za ufungaji nyingi zaidi.

Changamoto kubwa liko kwenye eneo lao la ushambuliaji wachezaji wa timu zote mbili wanaocheza eneo la ushambuliaji wamekuwa na chanagamoto ya kutumia nafasi, tofauti ni kuwa Yanga SC wamekuwa na wachezaji wengine nje ya washambuliaji ambao wamekuwa wakitumia vizuri nafasi wanazotengeneza jambo ambalo ni tofauti kwa upande wa Simba SC ambao wanatengeneza nafasi ila bado hazitumiki.

SOMA ZAIDI: Tabiri Sasa Matokeo Ya Dabi Ya Kariakoo Hapa Kijiweni

8 Comments

  1. 𝗧𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶 𝗔𝗯𝗮𝘀 on

    𝗞𝗮𝗺𝗮 𝗸𝗮𝘄𝗮𝗶𝗱𝗮 𝗱𝗼𝘇𝗶 𝗻𝗶 𝗶𝗹𝗲 𝗶𝗹𝗲
    𝘀𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗮𝗻𝗮𝗸𝘂𝗳𝗮 𝗴𝗼𝗹𝗶 2:0 𝗸𝗮𝘃𝘂 𝗸𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮 𝘁𝗮𝗮𝗯𝘂 𝗶𝗸𝗼 𝗽𝗮𝗹𝗲 𝗽𝗮𝗹𝗲 𝗯𝘆 𝗧𝗔𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗕𝗔𝗔𝗔𝗔𝗦

  2. Idriss Salif on

    Mchezo wa leo ni mrahisi kwa yanga maana presha ipo kwa mpinzani simba. Ataingia kwa presha ya kutaka kulipa kisasi, presha ya kuzuia kudhalilika tena kutokana na kichapo cha goli 5 kilichopita hatotaka kufungwa tena kiwango hiko cha mabao, presha ya ku pafom vibaya kulingana na fomu yake kutokuwa nzuri kwa michezo ya karibuni…. pamoja na presha ya kuona mpinzani akifanya vizuri ktk michezo ya karibuni. Usisahau na presha ya mwalimu Benchika, ndio game iliyomfungisha virago mwenzie Robertinho

  3. Rumbyambya Jr on

    Tight game..very tight game Lakini mechi itaamuliwa na atakae tumia nafasi. Kuipitq backing ya Yanga ni changamoto inahitaji seriousness na Accurate ya kutosha. Simba wasipishane na Yanga itawagharimu. Yanga wanaweza tengeneza Nafasi nyingi but wasitumie nafasi hizo wakatumia chache saana

Leave A Reply


Exit mobile version