Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuvuna alama 3 lakini haitakuwa rahisi kwao kwa sababu Mashujaa pia wanahitaji alama 3 ili kutoka chini ya Msimamo wa ligi kuu ya Nbc kwani Mashujaa wataingia na script ya Kagera Sugar na Dodoma jinsi ambavyo walikabiliana na Yanga, tutegemee na wao wakikaa nyuma kulinda zaidi huku wakitumia ile mipira ya kushtukiza zaidi yaani counter attacks.

Yanga wataingia kama timu ya kwanza kutokana na ubora wao hivyo wanapewa nafasi kubwa ya kuvuna alama lakini ugumu ninaouona ni jinsi gani Yanga wataweza kuifungua Mashujaa kwani tumeona dhidi ya Dodoma walivyopata tabu kuwafungua na hapa ndio msingi kamili wa kauli yangu kwanini hautakua mchezo mgumu.

Ukiwaacha yanga wakushambulie kwa muda mrefu basi tambua kuwa unawapa nafasi ya wao kupanga mipango yao ya jinsi ambavyo wanaweza kukufunga na hapa ndipo ambapo mchezo utakua mwepesi na rahisi zaidi kwa wananchi kwani timu kadhaa zilizokaa nyuma nyingi zimeshindwa kulinda na kukutana na kipigo cha dakika za jioni dhidi ya Yanga mfano hai unaweza kuona namna ambavyo Namungo ilivyokua lakini pia na Dodoma Jiji.

Kukosekana kwa Aziz ki kunaweza kukawa sababu ya Yanga kupata tabu sana kufunga mabao kama ilivyokuwa awali, hivyo leo nategemea kuwaona Maxi Nzegeli, Pacome, Guede na wengine kuonyesha ubora wao wa kufunga mabao na tusubirie kuona jinsi gani ambavyo makocha wat imu zote mbili jinsi ambavyo wameviandaa vikosi vyao ili kuibuka na ushindi wa mchezo huu muhimu kwa timu zote mbili.

SOMA ZAIDI: Simba Wasijiamini Kwa Ushindi Wa Tabora, Azam Ni Bora Sana

1 Comment

  1. Pingback: Simba Wamefikiria Kuhusu Mapato Au Alama 3 CCM Kirumba? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version