Timu zote mbili kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ngumu kwao kuwa na takwimu za wao kwa wao kutokana na hiyo ikisababishwa na kutokukutana kwa miaka ya hivi karibuni kabisa na hiyo imesababisha mchezo huo kutajwa zaidi nje Ya uwanja kuanzia Nyumbani na hata Afrika kwa ujumla.

Takwimu zao kwa michezo yao mitano ya mwisho kwenye michuano yote ambayo klabu hizo imecheza imekuwa na uwiano ambao unashabiana kwa kiasi Fulani ambapo Yanga SC katika michezo hiyo mitano imefanikiwa kushinda michezo mitatu na kupoteza michezo 2 na kwa upande wa Mamelod Sundowns wao wakishinda michezo minne na kutoa Sare moja huku wakifunga magoli 9 na wakifanikiwa kuruhusu goli moja tu na kwa upande wa Yanga SC wakifanikiwa kufunga magoli 10 na wakiruhusu magoli manne tu

Namna takwimu zilivyo zinaonyesha kuwa Mamelodi amekuwa na matokeo zaidi kuliko Yanga SC ila uzuri ni kuwa wamekuwa wanashabiana zaidi kwenye upatikanaji wa magoli ambapo Yanga amefunga 10 na Mamelod Sundowns akifunga 9 jambo ambalo linatoa uhalisia wa kushuhudia mchezo mzuri na magoli pia yakipatikana.

Mamelod Sundowns wamekuwa wakitumia zaidi mpira wa chini kwa kucheza mpira wa chini zaidi na wenye kasi pia na ilo limejengwa kwa kuwa na uimara zaidi kwenye eneo Lao la kiungo kuanzia eneo la kukaba na kushambulia pia jambo ambalo alinautofauti na Wapinzani wao Yanga SC ambao nao wamejijenga Zaidi kupitia eneo Lao la kiungo.

Upi ni ubora wa Mamelod Sundowns? Ni eneo Lao la kiungo ndiyo ubora wao ulipo na unabebwa hapo kuanzia kukaba na kushambulia pia. Yanga SC watumie mbinu gani kuwashinda Mamelod Sundowns? Hiyo ni kuwa na nidhamu kubwa ya kujilinda na kuwa Heshima wapinzani wao na kikubwa ni kuepuka kupishana nao sana bali kutumia zaidi “Caunter Attack” pamoja kuziba mianya Ya kutengeneza nafasi za kufunga kwao.

Kipi Mamelodi anaweza kuibuka na ushindi ? Moja Ya madhaifu makubwa ya Yanga SC ni pale wakikutana na timu ambayo inatumia zaidi maeneo yao ya pembeni “winga” wenye kasi kwa kutumia pasi fupi fupi.

Ubora wa Vikosi vyote viwili inapelekea kuwa na matarajio ya kushuhudia mchezo wa kupishana zaidi jambo ambalo ikitokea imekuwa hivyo basi magoli mengi yanaweza kuoatikana.

SOMA ZAIDI: Kuhusu Simba Nilitegemea Baada Ya Kumuona Mchezaji Huyu

1 Comment

  1. Pingback: Yanga Waligoma Kuingia Mtego Wa Mamelodi - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version