Klabu ya Yanga itashuka dimbani kukipiga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi hii Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam moja kati ya mechi ambayo bila shaka inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka wa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Iwapo Yanga watashinda nyumbani kwa ushindi wowote ule watakuwa na uwezekano mkubwa sana wa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali kwani hii ni kwa sababu Mamelodi Sundowns huwa hawana matokeo mazuri wakiwa kwao iwe katika dimba la FNB Stadium au Loftus Versfeld hasa kwenye hatua ya mtoano.

Mara nyingi Mamelodi Sundowns wametolewa nyumbani kutokana na matokeo ya ugenini ambayo wanakua wameyapata.

Mwaka jana bao la kujifunga la Mothobi Mvala liliwapa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Wydad Ac na kuishia nusu fainali baada ya kupata suluhu (0-0) ugenini.

2021/2022 Petro de Luanda alimtoa Mamelodi Sundowns palepale nyumbani kwake baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Petro kusonga mbele kwa jumla yaushindi wa mabao 3-2 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani

2021/2020 Al Ahly alimtoa Mamelodi Sundowns nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-1 baada ya kupata ushindi wa 2-0 Cairo. (alirudia alivyofanya 2019/2020)

2019/2020 Al Ahly alimtoa Mamelodi Sundowns nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-1 baada ya kupata ushindi wa 2-0 Cairo.

2019/2018 Mamelodi Sundowns alipasuka 2-0 ugenini dhidi ya Wydad akaenda kushinda 1-0 nyumbani na kutolewa.

2017 Mamelodi alifungwa 1-0 ugenini dhidi ya Wydad na kushinda 1-0 nyumbani kisha wakatolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Hata kwenye AFL Mamelodi alivuka hatua ya robo fainali baada ya kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Petro de Luanda na kutoa suluhu (0-0) nyumbani.

Kama Yanga watashinda ushindi wowote ule hapa nyumbani watakuwa na uhakika wa asilimia kubwa kusonga mbele.

SOMA ZAIDI: Mfumo Huu Utambeba Chama Kumuua Al Ahly Kwa Mkapa

1 Comment

  1. Pingback: Simba Wakifanya Hiki Wanamfunga Al Ahly Mapema Tu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version