Ukizungumzia michuano mikubwa kabisa ya mpira wa miguu ngazi za timu ya taifa huwezi kuacha kutaja fainali za kombe la dunia moja kati ya michuano ambayo huibua hisia nyingi kwa mashabiki wa soka duniani lakini kubwa zaidi kwa timu ambazo zitakua zimefuzu katika michuano hii. Na bingwa mtetezi wa michuano hii ni Argentina ambao walichukua ubingwa katika fainali zilizofanyika katika nchi ya Qatar mwaka 2022.
Wakati tayari inafahamika wazi kuwa michuano ijayo itafanyika katika bara la Amerika ni wazi kuwa kuna dondoo mbalimbali ambazo unapaswa kuzifahamu kuhusu michuano hii itakayofanyika katika majiji makubwa kabisa ya bara la Amerika likihusisha viwanja mbalimbali vya nchi ya Marekani,Canada na Mexico.
- Uzinduzi wa Kombe la dunia la mwaka 2026 utakua katika uwanja maarufu wa Estadio Azteca huko Mexico City siku ya Alhamisi, tarehe 11 Juni 2026 huku fainali imepangwa kufanyika Jumapili, tarehe 19 Julai 2026, huko New York New Jersey.
- Toronto, Mexico City, na Los Angeles ni miongoni mwa majiji ambayo yatashiriki kama wenyeji wa mechi za ufunguzi za timu zao za kitaifa.
- Canada, Mexico, na Marekani wamehakikishiwa kucheza mechi zao tatu za awamu ya makundi nyumbani huku Guadalajara, Vancouver, na Seattle pia wamechaguliwa kuwa wenyeji wa mechi za hatua ya makundi za nchi mwenyeji.
- Jiji la Miami litakuwa mwenyeji wa mechi ya kutafuta mshindi wa wa tatu, Dallas na Atlanta zitakuwa wenyeji wa nusu fainali, wakati Dallas itakuwa mwenyeji wa mechi tisa (9) – idadi kubwa zaidi kati ya Majiji yote ya Wenyeji kwenye mashindano.
Hatua ya makundi
- Siku ya kwanza ya mashindano itajumuisha mechi mbili, ikiwa ni pamoja na ufunguzi rasmi wa mashindano huko Mexico City na mechi nyingine huko Guadalajara.
- Siku ya pili itawahusisha waandaaji wa michuano hii ambao ni Canada na Marekani.
- Siku nne za mwisho za awamu ya makundi zitajumuisha mechi sita kwa siku. Mechi katika kundi moja zitachezwa kwa wakati mmoja ili kudumisha usawa wa mashindano.
- Siku zote zingine za awamu ya makundi zitajumuisha mechi nne kwa siku kwenye nyakati nne za kuanza tofauti.
- Estadio Azteca huko Mexico City unatarajiwa kuwa uwanja mwenyeji wa mechi ya ufunguzi kwa mara ya tatu ukiweka historia katika Kombe la Dunia la FIFA kama uwanja wa kwanza kufanya hivyo.
- Hii itakua mara ya kwanza kwa Canada kuwa mwenyeji wa michuano hii, likiongezea historia yake ya kufurahisha ya kuandaa mashindano makubwa ya FIFA kwa wanawake na vijana, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2015 lillilokuwa la kuvutia sana.
- Marekani itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA kwa mara ya pili, baada ya toleo la mwaka 1994 lenye rekodi. Marekani pia imeandaa matoleo mawili mafanikio ya Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA (1999 na 2003).
SOMA ZAIDI: Matokeo na Ratiba ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026 Barani Afrika
4 Comments
Pingback: Ratiba Ya Kufuzu Kombe La Dunia Kwa Timu Za Taifa Afrika
Hili la 2026 litakuwa zaidi ya lililopitaa,,
Tunaombaa latiba
Ratiba Ya Kufuzu Kombe La Dunia 2026 Kwa Timu Za Taifa Afrika
Ratiba Kamili Iko Hapa ➡️➡️ https://www.kijiweni.co.tz/ratiba-ya-kufuzu-kombe-la-dunia-kwa-timu-za-taifa-afrika/
Mtaa Unaongea