Meneja wa Barcelona, Xavi Hernandez amemsifu Marc Andre ter-Stegen kama mlinda mlango bora zaidi duniani.

Xavi alikuwa akizungumza baada ya ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye LaLiga Jumapili.

Matokeo hayo yaliifanya Barca kufikisha pointi 11 mbele ya Real Madrid inayoshika nafasi ya pili kwenye jedwali zikiwa zimesalia na mechi nane.

Ter Stegen pia alifikia rekodi safi ya Claudio Bravo ya mechi 23 katika msimu mmoja wa LaLiga.

“Marc André ter-Stegen ni miongoni mwa makipa watatu bora zaidi duniani na kwa sababu ya mchezo wetu nadhani yeye ndiye bora,” Xavi alisema baada ya mchezo huo.

Barcelona watakuwa ugenini kucheza na Rayo Vallecano siku ya Jumatano, Aprili 26.

Leave A Reply


Exit mobile version