Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangaza washindi wa vipengele mbalimbali vya Tuzo za msimu wa mwaka 2023 zikihusisha vilabu na timu za Taifa ambapo ikumbukwe kuwa walitangaza vipengele mbalimbali vinavyowaniwa katika Tuzo hizo.
Wafuatao ni washindi katika vipengele mbalimbali vya Tuzo hizo:
a) Klabu Bora Ya Mwaka
Wanaume : AL AHLY Kutoka nchini Misri
Wanawake : MAMELODI SUNDOWNS Kutoka nchini Afrika Kusini.
b)Mchezaji Bora Ligi Ya Ndani
Wanaume : Percy Tau Kutoka AL AHLY
Wanawake: Fatima Tagnout Kutoka AS FAR RABAT
c)Mchezaji Bora Chipukizi
Wanaume : Lamine Camara Kutoka Senegal
Wanawake : Nesryne El Chad Kutoka Morocco
d)Timu Bora Ya Mwaka
Wanaume : Morocco
Wanawake: Nigeria
e) Goli Bora La Mwaka tuzo imeenda kwa Mahmoud Kahraba
f) Golikipa Bora Wa Mwaka
Wanaume : Yassine Bounou Kutoka Morocco
Wanawake : Chiamaka Nnadozie Kutoka Nigeria
g)Kocha Bora wa Mwaka
Wanaume: Walid Regrarui Kutoka Morocco.
Wanawake: Desiree Ellis Kutoka Afrika Kusini.
h) Mchezaji Bora Wa Mwaka
Wanaume: Victor Osimhen Kutoka Nigeria na Napoli
Wanawake: Asisat Oshoala Kutoka Nigeria Na Barcelona
Kwa taarifa mbalimbali za michezo na makala endelea kuzisoma kwa kugusa hapa.
1 Comment
Pingback: VICTOR OSIMHEN Mchezaji Bora Afrika. - Kijiweni