Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kiasi kuizungumzia klabu ya Simba moj kati ya mashabiki wakubwa na mbunge Hamisi Kigwangalla ameibuka na waraka mzito kuhusiana na yale yanayoendelea ndni ya viunga vya Msimbazi na waraka huo kauandika hivi,

“Labda mpeni timu Kigwangalla…” ni kauli ya mwanaYanga mmoja kwenye clip inayozunguka ‘virally’ mitandaoni. Mwishoni wanacheka kwa mzaha na dharau kama vile mimi kupewa timu Ya Simba ni mzaha fulani hivi!

Iko hivi; siyo kwamba sina uwezo wa kuiongoza Simba kwa mafanikio makubwa zaidi ya haya, ama sina uwezo wa kuinunua Simba ama kununua hisa za Simba. NAWEZA SANA!

Inawezekana sina hiyo pesa kwenye akaunti zangu, lakini nina taarifa na maarifa ya wapi naweza kupata hizo pesa na kuinunua Simba! Ukiwa na ‘mindset’ ya kimaskini na hauna maarifa utaona mtu kama mimi siwezi kununua mali ya TZS 20bn. Waswahili huwa tunajidharau sana kwa sababu utumwa umegoma kutoka vichwani mwetu.

Binafsi, niliikataa hii ‘slavery mindset’ nikiwa mdogo sana, ndiyo maana mimi na wenzangu tuliweza kununua kampuni kubwa kabisa ya kununua mazao yenye thamani ya zaidi ya bilioni 7 wakati ule (mwaka 2007), nikiwa na umri wa miaka 32, tena nikiwa ‘nobody’ na sina ‘network’ yoyote ile (kama nilivyo leo!).

Sema kwa sasa hivi siwezi kusema nanunua Simba, siyo kwa sababu sina uwezo wa kuinunua lakini ni kwa sababu ya kuepuka ‘conflict of interest’ (mgongano wa kimaslahi) maana nimekuwa mkosoaji mkubwa wa jinsi mchakato huu ulivyoendeshwa, na kimaadili siyo sawa kutamani kuwa na hisa maana itaonekana kumbe kelele zangu zote ni kwa sababu nilikuwa nina wivu na mwekezaji wa sasa.

Halafu, niwaambieni kitu Simba ni brand kubwa nchini na Afrika kwa sasa. Na inazidi kukua. Ikiwekwa mifumo mizuri ya usimamizi na ya kifedha, wanunuzi wa Simba hawawezi kukosa kujitokeza.

Sasa hivi kila mtu anaogopa kuingia humo, haswa baada ya kuona figisu figisu zilizopo na kutokamilika kwa ‘transaction’ ya manunuzi na huyu mwekezaji wetu kwa zaidi ya miaka 6 leo!

Ukitaka kuona Simba inapata wawekezaji wengi na wazuri ni lazima uweke “MUUNDO” mzuri wa utawala na usimamizi wa club; aidha uwe na “MUUNDO” mzuri wa umiliki wa hisa za Simba.

Mfano: kwa nini Mwenyekiti wa Club (anayetokana na wanachama) na Mwenyekiti wa Bodi (anayeteuliwa na mwekezaji) wasiwe wanapokezana cheo Cha Rais wa Club na Makamu wa Rais wa Club (say kila baada ya miaka mitatu)? Na kwamba Rais akiwa ni Mwenyekiti wa Club ya wanachama basi Mwenzake automatically anakuwa Makamu na vice versa! Na kwa vyovyote vile anayekuwa Rais anakuwa na mamlaka yote!

Ama, ni kwa nini mwekezaji awe mmoja? Kwa nini tusiseme – asilimia 49 ya hisa za Simba ni lazima zimilikiwe na wawekezaji wasiopungua watatu na kwamba hakuna mwekezaji mmoja kuwa na hisa zinazozidi 20%, na wawekezaji pengine wasizidi idadi fulani?!

Ukirekebisha haya na ukasema hisa hizi zitauzwa kwa zabuni za siri za “USHINDANI”, utaona watajitokeza wawekezaji wengi na hisa zitauzwa kwa bei kubwa zaidi maana watapigana vikumbo pale!

Na ukisema unaweka wazi mikataba yote ya matangazo ya bidhaa, mauzo ya merchandise, migao ya viingilio, manunuzi ya wachezaji, makocha na waajiriwa wengine! Unachapisha hesabu kwenye majarida ya wazi; utaona watu wengi watajitokeza kuwekeza!

Muhimu: kuwe na nia njema na ya kweli ya kutaka kuleta mageuzi ya kweli ya uendeshaji wa club na siyo janja janja ya wachache waliogeuza club chanzo chao cha kujipatia ‘maisha’ ama kukuza ‘brand’ zao binafsi.

Mdau wa KIJIWENI wewe una lipi la kusema? Tuambie kwenye comment hapa chini

22 Comments

  1. Ni akili kubwa sana inatakiwa kutumika ili Simba wamweleee huyu jamaa tangu zamani alishaona vile ambavyo Simba inapotea alipouliza tyu akaambiwa msaliti sisi watu weusi bado hatuaminiani wewe jaribu kuanzisha mchakato wote wa mabadiliko mahali Fulani utaambiwa unataka jambo Fulani

    Mm Imani yangu Africa tungemua kutumia akilizi zetu halisia hakika hao tunaowaita weupe Kila siku wangekuwa kwetu kujifunza

    Unaenda marekani kujifunza mfumo Fulani unakuta waalimu hasa ama waanzilishi ni watu kutoka bara la Africa

    Angalia wacheza soka, angalia viongozi mashuhuri wengi ni weusi, Nenda kwenye Vipaji vikubwa vya Music why tuna akili ya kubebewa

    Uhalisia alichokisema kigwangala hakuwezi kutekelezwa kwa sababu wengi wanataka faida kwanza kuliko manufaa ya timu kwa miaka mia mbili ijayo

  2. Kidullahson HL on

    Sema kigwangala ana point sana, muundo wa simba sc sio rafiki kabisa, leo hii mangungu ni Mwenyekiti wa wanachama wanaomiliki hisa asilimia 51% lakini wanaoonekana na kupewa heshima ni viongozi wa mwekezaji, Mangungu apewe heshima yake please, mambo ya rais wa heshima 🌚🌚 tungeachana na mambo ya uchawa, watu wapewe majukumu wachape kazi.
    Afu pia kuhusu uwekezaji Yanga wamefanya vizuri sana, sio vibaya kuiga mambo mazuri 😃😃 Simba nao waige tu, systems yaku recruit wachezaji nayo ibadilishwe, kila mwaka wanaleta wachezaji ambao hawana input kwenye timu mwisho wa mwaka wanaanza kubanana kuvunja mikataba 🙅‍♂️🙅‍♂️

  3. Alichoandika kigwangala yupo sahihi kabisa lakini kwawasio na uelewa bado wataponda tatizo lililopo hao viongozj hapo waliopo kula yao ipo hapo haiwezekani mwenyekiti wa club hana PAWA kwenye anakua kama mtumwa nawakati yeye kashikilia hisa asilimia 51 za wanachama huyu mwenye asilimia 49 ndio mwenye nguvu

  4. Alexander INVESTMENT on

    Simba sc kuna shida kubwa tena sana..upande wa viongozi…hata mhindi wetu nae n mjanja mjanja tu..na huwa anaibuka wakati wa changamoto ya matokeo anapoozesha upepo kwa maneno then anapiga kimya..inawezekana hata pesa ya usajili hatoi ya kueleweka..lakn pia udalali ni mwingi ndani ya timu

  5. Naitamani sana simba ya manara na babra irudi kisha mangungu na jaribu tena ( try again ) waondoke simba tena wasiruhusiwe hata kuingia uwanjani wakati simba inacheza🙄

  6. Angeongea kiingereza ndo wabongo tungemzingatia ila point hata iwe nzito kivipi ila ukawa tu kwa kiswahili wabongo hatunaga muda nayo 😔😔😔
    ” Kitu cha hovyo kikisemwa kwa lugha ya kigeni kitaonekana cha maana sana ” alisikika baba WA taifa Mwl Nyerere J. K

  7. 𝗧𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶 𝗔𝗕𝗕𝗔𝗦 on

    Kigwangara Hana uwezo wa kuimiliki 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔. Wala 𝘀𝗶𝗺𝗯𝗮 haina matatizo saaaaana sema tu ni suala la mda watajipata tu wasife moyo,kinachotakiwa warekebishe pale wanapoona panavuja 𝗺𝘀𝗶𝗺𝘂 ujao na wao wafanye vizuri.

    by 𝘁𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶 𝗔𝗕𝗕𝗔𝗦.

  8. Pingback: Pale Simba Shida Sio Mangungu Ni Wachezaji Hawa - Kijiweni

  9. Pingback: Mchezaji Gani Wa Nje Hapa Ligi Kuu Amekuwa Bora Zaidi Kwako? - Kijiweni

  10. Pingback: Viongozi Simba Wanajiroga Wenyewe Na Kujitega Mtego Mbaya - Kijiweni

  11. Shida hipo pande zote mbili:
    *Kwanza upande ea muwekezaji, yani huyu MO cjui tuseme hajui majukumu yake au lah mana amewaamini xana hao viongoz wake kina mangungu na amewaachia mamlaka yote ya usimamizi wa timu yeye akiwa bize na biashara zake binafsi.
    *Pili ni hawa viongozi, mangungu na mwenzake “try again” wanautumia vibaya uhuru waliopewa na kugeuza taasisi kama sehemu yao ya kuingiza vipato vyao binafsi ndo mana wanaondoka wachezaji wazuri kina baleke na kina phiri tunaletewa kina jobe.

Leave A Reply


Exit mobile version