Mashabiki wa soka wa klabu ya Yanga bila shaka kabisa katika hatua hii ya 16 bora katika michuano ya AFCON watakua na kipengele kikubwa sana cha kuamua katika kumpa sapoti mchezaji gani kati ya Aziz Ki wa Burkina Faso na Djigui Diarra wa Mali ambao timu zao za Taifa zimefuzu hatua hii muhimu na ubaya zaidi ni kuwa wanakutana katika raundi hii katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Amadou Gon Coulibaly.

Ukimtazama mchezaji Djigui Diarra ambaye tangu kuanza kwa michuano ya mwaka huu ya mataifa ya Afrika amemuaminisha kocha mkuu wa timu hiyo ambapo ameanza katika mechi zote za makundi ambapo ameruhusu bao moja pekee katika mchezo dhidi ya Tunisia ambao walitoka sare ya bao 1:1.

Aziz Ki ameanza katika michezo miwili akiwa hajafunga bao hata moja katika michuano hii lakini ameonesha kile ambacho kimemfanya kocha mkuu wa Burkina Faso kumuita katika kikosi hicho mwamba huyu wa Ouagadougou.

Ikumbukwe kuwa mshindi wa mchezo wa Burkina Faso dhidi ya Mali anatinga hatua yar obo fainali sasa nadhani kwa mashabiki wa Yanga itakua ni siku ngumu kabisa ya kuchagua nani wampee sapoti ili aweze kutinga hatua ya robo fainali ya AFCON kwa mwaka huu.

Kitendo cha wachezaji hawa wawili kutoka katika klabu ya Yanga kukutana katika mchezo huu ni moja kati ya sehemu ya wao kujitambulisha kimataifa na kuonekana zaidi katika ulimwengu wa soka kwani kupitia michuano hii wapo maskauti na mawakala wat imu kubwa wanaotafuta vipaji vipya.

Kufika hatua ya 16 bora kwa wachezaji hawa wawili tena wakiwa wanachezea klabu ya Yanga ni wazi kuwa lazima kuna mchezaji kutoka kwa wananchi ambae anaingia robo fainali katika AFCON yam waka huu.

Ukiachana na wachezaji hao wa Yanga, klabu ya Simba wao watakuwa na utulivu wakimtazama staa wao beki Henock Inonga akiwa na taifa lake DR Congo Januari 28 saa 5:00 usiku atakapokuwa na vita ya soka dhidi ya Misri isiyotabirika. Endapo Congo itafuzu hatua hiyo mbele ya Misri itakwenda robo fainali kukutana na mshindi wa mchezo wa majirani kati ya Guinea ya Ikweta dhidi ya Guinea Bissau mechi ambayo itapigwa Januari 28 saa 2:00 usiku.

SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya AFCON Hatua Ya 16 Bora

1 Comment

  1. Pingback: Waliofanya Vizuri Hatua Ya Makundi AFCON - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version