Wiki moja iliyopita ilionekana kana kwamba Ivory Coast wangefungasha virago katika hatua ya makundi katika michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) inayochezwa nchini mwao, lakini sasa wametinga robo fainali baada ya kuwabwaga Senegel kwa penalti 5 kwa 4 baada ya mchezo huo kumalizika dk 120 ubao ukisoma 1 -1.

Tembo wamewaduwaza watu wengi kwani walimaliza hatua ya makundi na rekodi mbovu ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu kwenye makundi, baada ya kukamilisha duru ya kwanza na kichapo cha fedheha cha 4 – 0 kutoka kwa kwa Guinea ya Ikweta moja kati ya kichapo kizito kabisa kuwahi kuwakumba katika ardhi ya nyumbani jambo ambalo lilipelekea kutimuliwa kwa kocha mkongwe wa Kifaransa Jean-Louis Gasse.

Wakati wengi wakiwa hawana Imani na uwezo wa Ivory Coast mbele ya Senegal lakini tumeona namna ambavyo wamebadilika mnooo na kuwanyanyasa vya kutosha timu ya Senegal na hii ni kwasababu ya uwepo wa kocha mpya ambaye ni mchezaji wa zamani Emerse Fae kwa kupewa mkataba wa muda.

Bila shaka ungekua usiku mzito sana kwao baada ya kukubali goli la mapema zaidi dakika ya 4 ya mchezo lakini walitulia na baadae kupata penati iliyowainua upya na kuwafanya warejee mchezoni tunaona umuhimu sasa wa kuwa na wachezaji wakomavu kwani ukiwa na wachezaji ambao hawana ukomavu huo kumbuka kuwa watacheza na presha kubwa jambo ambalo litaufanya mchezo kuwa mgumu kwao.

Unaweza usiamini lakini fikiria moja kati ya timu ambayo ilikua na matazamio makubwa ya kuwa inaweza kumaliza michuano hii kama mabingwa tena lakini wakipoteza nafasi hii licha ya kuwa timu iliyofanya vizuri zaidi katika hatua ya makundi kwa kushinda mechi zake zote 3 huku Ivory Coast wao wakiwa wameshinda mechi 1 na kusare 1 huku wakifungwa 2 lakini wakiendelea nah atua inayofuata ya robo fainali ya AFCON.

SOMA ZAIDI: DR Congo Kumtoa Egypt Haijanishangaza Nilitegemea

1 Comment

  1. Pingback: Ratiba Kamili Ya Robo Fainali AFCON 2023 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version