Michuano ya mataifa barani Afrika msimu huu imekua na mambo mengi ya kustaajabisha haswa kutokana na matokeo yaliyokua yakitokea lakini pia na maamuzi ya waamuzi katika michuano hii mikubwa zaidi barani Afrika kwani imekuwa jukwaa la kuonyesha maendeleo makubwa ya teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR) katika mchezo wa soka. Matumizi ya VAR katika AFCON yameleta mabadiliko chanya na kufundisha namna bora ya kutumia teknolojia hii.

Matumizi ya VAR katika michuano hii yamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha haki na uadilifu katika matokeo ya mechi kwani wachezaji, mashabiki, na viongozi wa timu wameweza kuona namna ambavyo maamuzi yalivyokua mpaka kutendeka kwa maamuzi ya mwisho  na Imani ambayo ilikua juu kuwa maamuzi yanayofanywa na waamuzi yanasimamiwa kwa haki na kwa usahihi jambo ambalo limepelekea kuzuia kasoro za kibinadamu ambazo zinaweza kutokea wakati waamuzi wanategemea maamuzi yao pekee.

Kuanzia hatua ya makundi mpaka kufikia hatua hii ya 16 bora bila shaka tumeshuhudia jinsi VAR inavyoweza kuzuia makosa makubwa ya uamuzi.Ikiwa ni kwa kuchunguza makosa ya kuotea, mikwaju ya adhabu, au matukio mengine muhimu uwepo wa teknolojia hii umeweza kusaidia kurekebisha makosa ambayo yangeweza kuwa na athari kubwa kwenye matokeo ya mechi.

Katika ligi mbalimbali kubwa barani Ulaya kumekua na changamoto ya muda kupotea kutokana na teknolojia hii ya VAR lakini katika michuano ya mwaka huu kulikua kuna hofu kwamba matumizi ya VAR yanaweza kuchukua muda mrefu na kuathiri kasi ya mchezo jambo ambalo sio kweli kwani imewafundisha watu jinsi ya kuitumia kwa ufanisi zaidi kwani kumekuwa na utaratibu mzuri wa kutumia VAR na kutoa mafunzo kwa waamuzi kumewezesha kufanya maamuzi kwa haraka na kwa usahihi.

Nadhani sasa kwa maamuzi ambayo yamekua yakitolewa katika AFCON ni fursa kwa wadau wa soka kuelewa jinsi VAR inavyofanya kazi na kwa nini ni muhimu. Kupitia maamuzi ambayo yamekua yakitolewa katika michezo mbalimbali kuanzia hatua ya makundi mpaka hatua hii ni wazi kuwa  mashabiki, wachezaji, na viongozi wa timu mbalimbali wamepata uelewa zaidi kuhusu jukumu la teknolojia hii katika kuboresha soka.

SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya AFCON 2023 Hatua Ya Robo Fainali

3 Comments

  1. Pingback: Andre Onana Kutoka Kukatazwa Kucheza Mpira Mpaka Ubilionea - Kijiweni

  2. Pingback: Inonga Amejiuza AFCON Sitashangaa Akiondoka Simba - Kijiweni

  3. Pingback: Hakuna Mnyonge Yoyote Anaweza Kuwa Bingwa AFCON 2023 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version