Wakihitaji kuchukua ubingwa wa 4 katika historia ya timu yao ya taifa hii leo Nigeria wako kibaruani katika fainali ya AFCON dhidi ya wenyeji wa michuano hii Ivory Coast moja kati ya mechi kubwa ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa sana Afrika.

Wakati masaa yakiwa yamebakia kwa ajili ya kushuhudia kandanda hii kutoka kwa wababe hawa wa soka barani Afrika kumbuka kuwa michuano ya msimu huu yamekua ya kuvutia na yenye tofauti kubwa sana kutokana na kuwa wengi waliamini katika mataifa makubwa ingawa yapo ambayo hayakufanya vizuri msimu huu.

Tumekuandalia hapa orodha ya wachezaji watano ambao wanaweza kuwapa ubingwa timu ya taifa ya Nigeria:

Stanley Nwabali

Ukiuzungumzia ukuta wa ulinzi wa Nigeria huwezi kuacha kumtaja golikipa Stanley Nwabali ambae amekua na kiwango bora katika michuano ya AFCON msimu huu ambapo ameruhusu bao 1 pekee katika michuano ya msimu huu. Anakitumikia kikosi cha Chippa United cha Afrika Kusini ambapo pia aliwaondoa kwa kuokoa penati zao.

William Troost-Ekong

Huyu ni kapteni wa timu ya taifa ya Nigeria ambae amekua na kiwango bora huku akivutia timu kadhaa za uarabuni zikimhitaji kwenda kucheza huko kutokana na kiwango bora alichokionesha msimu huu. Ni moja kati ya wachezaji amabao nao wanai ngia katika orodha hii ya wacheaji wa Nigeria wanaoweza kuwapa ubingwa Nigeria.

Victor Osimhen

Mchezaji bora wa bara la Afrika msimu huu ambaye katika michuano hii ana bao moja pekee amekua na mchango mkubwa kwa timu yake ya taifa akiwa na kasi na nguvu kubwa katika kushambulia jamboa ambalo linawapa nafasi wachezaji wengine kufunga. Bila shaka kwa sasa anachowaza ni namna gani ambavyo atachukua ubingwa nakuendelea kuweka rekodi zake binafsi na taifa lake kwa ujumla.

Ademola Lookman

Huyu ni mtu hatari kabisa wa kikosi cha Nigeria kwani amekua na kiwango bora katika michuano hii huku akifunga mabao kadhaa katika michuano ya msimu huu. Mpaka sasa ana mabao 3 akiwa na kasi na uwezo mkubwa wa kuchezea mpira.

SOMA ZAIDI: Wachezaji Watano Muhimu Wa Kuwapa Ubingwa Ivory Coast

Leave A Reply


Exit mobile version