Wakati wengi wakisubiri kutazama fainali ya michuano ya mataifa barani Afrika ambayo inawakutanisha wenyeji Ivory Coast dhidi ya Nigeria kumekua na wachezaji wengi ambao wamekua wakijadiliwa kuwa wanaweza kuwapa ubingwa tembo wa Ivory Coast?  na hii ni kutokana na namna ambavyo timu hii mpaka kufika hatua hii ya fainali ilivyokua imepitia katika nyakati ngumu na haswa baada ya kupita kama best looser.

Tumekuandalia hapa idadi ya nyota watano wa kuchungwa ambao tunaamini wakiwa vizuri hii leo uwanjani basi wanaweza kuwapa ubingwa timu ya taifa ya Ivory Coast jambo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na waivory coast wanaojaa sana kwenye mechi zinazohusu timu yao ya Taifa.

Kumbuka kuwa Ivory Coast wakifanikiwa kuchukua ubingwa huu basi utakua ubingwa wao wa tatu wa michuano ya AFCON.

Sebastian Haller

Alianza kuitumikia timu ya taifa ya Ivory Coast katika michuano hii kuanzia hatua ya mtoano na amekua na mchango mkubwa katika timu yake ya taifa akiwafungia bao zuri kabisa dhidi ya DR Congo lilowapeleka hatua ya fainali na amekua akionesha namna gani ni hatari zaidi anapokua katika lango la timu pinzani huku akiwa mkali zaidi katika mipira ya vichwa kwani ni mrefu na ana uwezo mkubwa wa kuruka.

Seko Fofana

Huyu ni kiungo wa Al Nasrr kutoka ligi kuu ya Saudi Arabia na amekua na kiwango kizuri pia katika michuano hii akiwa na kasi kubwa katika kushambulia na kukaba katika timu ya taifa ya Ivory Coast.

Katika michuano ya mwaka huu ameingia katika  kumbukumbu za kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao ambapo alifunga katika mechi ya Ufunguzi nab ado anataka kuendelea kuonesha kuwa bado yeye ni bora ana anaweza kuisaidia timu yake kuwa bingwa na kuubakisha ubingwa nyumbani.

Serge Aurier

Akiwa na miaka 31 ameendelea kuonesha namna alivyo mzoefu pale anapopata nafasi katika kikosi cha Ivory Coast akiwa ndani na hata nje ya uwanja. Kupitia uzoefu wake ameendelea kuwa msaada mkubwa kwa kocha wa Ivory Coast. Ameshacheza fainali kadhaa na anajua umuhimu wa fainali haswa katika uwanja wa nyumbani.

Simon Adingra

Licha ya kutopewa nafasi mwanzo ila ameendelea kuonesha namna gani ni hatari katika michuano ya AFCON msimu huu na alivyo hatari katika kushambulia na kuisaidia timu yake ya taifa katika hatua ya robo fainali n ahata ile ya nusu fainali.

Franck Kessié

Huyu ni kiungo mkongwe ambaye ameonesha namna gani alivyo bora katika michuano hii kanzia mwanzo mpaka hatua hii waliyofikia na kumbuka goli lake la dakika za jioni hatua ya 16 bora lilivyowarudisha katika kupambania best looser.

Kutokana na ubora alionao Kessie itakua njia muhimu kwake kuisaidia timu yake ya taifa na kuwa mabingwa wa AFCON.

SOMA ZAIDI: Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika

2 Comments

  1. Pingback: Wachezaji Watano Wa Kuwapa Ubingwa Nigeria - Kijiweni

  2. Pingback: Hawa Ndio Washindi Wa Tuzo Za AFCON Vipengele Vyote - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version