Ligi kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) imeendelea kushika hatamu na rekodi mblimbali zikiendelea kuwekwa katika ligi hiyo. Mpaka sasa anayeongoza ligi ni Azam Fc akiwa amecheza michezo 12 na alama zake 28 huku Mtibwa Sugar akishika mkia na alama zake 5 katika mechi 12 alizocheza.

Zipo rekodi mbalimbali ambazo mpaka sasa zinaendelea kuwekwa lakini hapa tutazame wachezaji waliofunga mabao ya mapema zaidi katika msimu huu mwaka 2023/2024 katika ligi kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).

SOSPETER BAJANA :Anashikilia rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi mpaka sasa msimu huu mwaka 2023/2024 akifunga goli sekunde ya 54 kwenye mchezo uliowakutanisha Azam Fc dhidi ya JKT Tanzania uliomalizika kwa AZAM Kushinda mabao 2:1.

YASSIN MGAZA :Alifunga bao dakika ya kwanza tu ya mchezo kwenye mechi iliyowakutanisha Tabora United dhidi ya Dodoma Jiji mchezo ambao Tabora aliondoka na ushindi wa mabao 2:1 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.

AWESU AWESU:Huyu ni kapteni wa wakusanya mapato wa Kinondoni ( KMC) alifunga goli dakika ya 1 tu kwenye mchezo uliowakutanisha KMC dhidi ya Mashujaa katika uwanja wa Uhuru. Matokeo yakiwapa faida Kmc wakiibuka na ushindi wa mabao 3:2.

ZIDANE SERERI :Mchezaji huyu wa Dodoma Jiji alifunga goli kwenye mchezo uliowakutanisha Dodoma Jiji dhidi ya KMC katika uwanja wa Uhuru ambapo alifunga goli dakika ya 2 ya mchezo.

FEISAL SALUM :FEITOTO alifunga goli dakika ya 2 ya mchezo katika mechi iliyowakutanisha AZAM dhidi ya Tabora United katika uwanja wa Azam Complex. Mchezo ambao ulimalizika kwa Azam kuondoka na ushindi wa mabao 4:0.

PACOME ZOUZOUA :Zidane wa Ivory Coast kutoka kwa Wananchi alifunga bao la mapema zaidi katika mchezo ambao Yanga walipoteza kwa bao 2:1 kutoka kwa Ihefu katika uwanja wa Highland Estate. Pacome alifunga goli dakika ya 3 ya mchezo.

KENNEDY MUSONDA :Alifunga goli dakika ya 3 ya mchezo uliowakutanisha watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ulioisha kwa matokeo ya Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 5:1.

Soma zaidi kuhusu ligi kuu Tanzania Bara kwa kugusa hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version