Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard amewasuta wachezaji wenzake kwa kufanya mambo ya “kijinga” wakati wa sare ya 2-2 na West Ham Jumapili.

Gabriel Jesus na Odegaard walifungia The Gunners kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa London Stadium.

Hata hivyo, Thomas Partey alipoteza mpira, jambo ambalo hatimaye lilisababisha Gabriel Magalhaes kufunga penalti katika kipindi cha kwanza. Benhrama alifunga na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Bukayo Saka kisha akakosa penalti mapema katika kipindi cha pili, muda mfupi baada ya Wagonga nyundo kusawazisha kupitia Jarrod Bowen.

“Tuliwapa kidogo mchezo waliotaka. Tuliwapa matumaini wakati walikuwa wamekufa kimsingi. Ni juu yetu.

“Tulianza kufanya mambo mengi ya kijinga na mpira na tukawaacha wacheze mipira mirefu, walipata mipira mingi ya kutupwa na kona na tukawaacha wacheze kwa sifa zao,” Odegaard alisema.

Leave A Reply


Exit mobile version