Ladha za ligi kuu zinaendelea na tumekua tukiona matokeo tofauti tofauti ambayo yamekua yakijitokeza katika mechi mbalimbali bila kusahau vipaji kadha wa kadha kutoka timu tofautitofauti zinazoshiriki ligi kuu.

Kumekua na wachezaji mbalimbali ambao wamekua na balaa lao katika ligi kuu ambao wamekua na viwango bora sana bila kusahau kuwa hatari wanapokua wako katika lango la timu pinzani na hapa tumekuandalia orodha ya wachezaji hatari wa kutazamwa kwa jicho la 3 pale unapowaona katika mchezo wa ligi kuu.

Feisal Salum “Fei Toto”

Mzaliwa wa Zanzibar, Tanzania akiwa anakitumikia kikosi cha Azam FC akiwa na miaka 26 akihudumu zaidi kwenye eneo la kiungo mshambuliaji. Feitoto kwa msimu huu amekuwa na kiwango kizuri na kuelekea mchezo wa Mzizima Derby dhidi ya Simba SC ni moja kati ya wachezaji wachache wa kuangaliwa kwenye mchezo huo. Amehusika kwenye magoli 12 ambapo amefanikiwa kufunga magoli 8 na kutengeneza mengine “Assist” 4 na hayo ni katika michezo 13 aliyocheza.

Saido Ntibazonkiza

Ni mzaliwa wa Bunjumbura nchini Burundi akiwa na umri wa miaka 36 akiwa ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Amecheza jumla ya michezo 12 na amehusika kwenye magoli 6 akifunga magoli 5 na akitoa pasi za magoli “Assist” 1 hata hivyo kwenye magoli hayo aliyofunga amefunga magoli 4 kwa mkwaju wa penalti. Nje ya kushambulia Ntibazonkiza amekuwa akihusika kwenye kusaidia kukaba amekuwa akikabia kuanzia juu eneo la ushambuliaji, sehemu ambayo amekuwa hatari zaidi ni swala la kupiga penalti.

Prince Dube

Amezaliwa Harare nchini Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 26 ni mshambuliaji wa Azam FC. Amehusika kwenye magoli 7 na hayo amefunga tu bila kutengeneza au kutoa pasi ya goli kwa mwingine. Prince Mpumelelo Dube amekuwa na bahati sana pale ambapo anapata nafasi ya kucheza kwani kwenye michezo 3 mfululizo amefanikiwa kufunga magoli 3.

Pascal Msindo

Anacheza nafasi ya beki wa kushoto msimu huu amekuwa na kiwango bora sana na licha ya kucheza kama beki ila amehusika kwenye magoli  4 ambayo ameyatengeneza kwa kutoa pasi za magoli. Kijana anayepata nafasi ya kucheza mbele ya mchezaji wa kigeni Cheikh Sidibe.

Stephane Aziz Ki

Amekuwa muhimili mkubwa sana kwa upande wa Yanga SC kwa msimu huu na ameshachangia jumla ya magoli 12 akifunga magoli 10 na kutoa pasi za magoli 2. Aziz Ki amekuwa hatari sana kwenye mipira ya faulo “Free Kick” hivyo ukicheza faulo eneo la goli lako na Aziz Ki yupo basi kuna asilimia kubwa akakuadhibu.

Kouassi Attohoula

Beki wa kulia wa Yanga SC ndiyo beki anayeongoza kwa kutoa pasi za magoli “Assit” akifanya hivyo mara 6 amekuwa akifanya majukumu yake mama ya kukaba kwa usahihi na pia amekuwa akihusika kwenye kushambulia. Ukikutana naye lazima uweke tahadhari naye amekuwa akipanda na kushuka kutengeneza nafasi za magoli kwa kiasi kikubwa.

Kipre Junior

Ni moja ya mawinga hatari wanaopatikana ndani ya Ligi kuu ya NBC amekuwa na hatari sana akiwa kwenye nusu ya mpinzani na hicho kimepelekea kuwa kinara wa kutengeneza magoli “Assit” akifanya hivyo mara sita (6) na akifunga magoli 4 hivyo kumfanya kuwa kati ya wachezaji wachache waliyohusika kwenye magoli ndani ya NBC. Kipre Junior ni winga hatari hususa kwenye 1v1 amekuwa na matumizi mazuri ya ufundi aliyonayo kuficha mpira ukikutana naye yapaswa kuwa makini sana.

Waziri Junior

Moja ya msimu bora sana kwa mshambuliaji huyu wa KMC FC msimu huu amehusika kwenye magoli 7 na hayo amehusika kwa kuyafunga. Amekuwa mtulivu sana eneo la mwisho na ni moja ya wachezaji wachache waliyotumia vizuri makosa ya wapinzani kufunga magoli muhimu kwa timu yake.

Max Nzengeli

Alianza msimu vizuri sana na ni mchezaji anayekimbia sana kiwanjani nje ya kuhusika kwenye magoli 10 kwa kufunga 8 na kutengeneza 2 ila amekuwa ni mchezaji anayesaidia eneo la ukabaji kwa kupanda na kushuka.Kiufupi ana mapafu kweli kweli ya kusaidia kukaba na kutekeleza kazi yake mama ya kushambulia eneo la mpinzani.

Emmanuel Mtambuka

Ni usajili mpya wa dirisha dogo kwenye kikosi cha Mashujaa FC amesajiliwa kutokea Stand United ya Championship lakini mpaka sasa ameshafanikiwa kufunga magoli 2 kwenye michezo yake 2 ya Ligi kuu ya NBC. Mshambuliaji hatari na bado ni kijana mdogo alipokuwa Stand Utd alikuwa akiongoza kwa magoli akifunga 9 na kutengeneza 4 ni tatizo lingine kwa mabeki na kipa ndani ya Ligi kuu ya NBC.

Marouf Tchakei

Kiungo huyu mshambuliaji amekuwa bora sana kwenye mipira ya pili hususa nje ya 18  ya lango la mpinzani maeneo hayo akipata nafasi huwa anatumia vizuri alianza kwa kuhitumikia Singida Fountain Gate ila kwa sasa yuko Ihefu FC. Ameshahusika kwenye magoli 8 akitengeneza magoli mawili huku akipachika kambani magoli 6.

Kibu Denis

Hana takwimu mzuri za kufunga au kutengeneza magoli ila ni moja ya mchezaji muhimu sana kwa Simba SC ana nguvu sana na huwa hampi nafasi mpinzani hususa anayekuwa akicheza naye eneo au upande mmoja naye. Amekuwa mtulivu sana na mali huwa inatulia mguuni kasi anayo na ana energy sana ni moja ya wachezaji wachache kwenye Ligi kuu ya NBC ambao kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho bado wanakuwa na energy ya kutosha anapanda kusaidia mashambulizi kama kazi yake lakini pia huwa nashuka chini kusaidia kukaba.

Khalid Aucho

Huyu ni kama ndiyo injini ya Yanga SC hausiki sana kwenye takwimu ila kazi yake ni kubwa sana kiwanjani amekuwa akiituliza timu vizuri kuanzia upigaji wake pasi. Nguvu anayo na imekuwa silaha yake kubwa sana anapokuwa na mali mguuni basi ni ngumu kupoteza ila pia pasi anazopiga huwa zinafika kwa wahusika. Awapo kiwanjani kikosi chake cha Yanga SC kinatulia sana na hiyo ni kutokana na utulivu aliyonayo awapo na mpira na hata wakati mpira ukiwa kwa mpinzani ni Mchezaji kiongozi ndani ya uwanja.

Ibrahim Bacca

Huwa ana mechi ndogo wala kubwa awapo kiwanjani basi kazi yake kubwa ni kutekeleza majukumu yake inavyotakiwa ni moja ya mabeki bora wa kati kwa sasa, ana kasi mtulivu na anacheza kwa jihadi sana pia ni mzuri kufanya recover kufanya tackling pamoja na mipira ya juu kiufupi yuko vizuri mipira ya juu na ya chini mshambuliajo yoyote yule akikutana naye lazima awe vizuri.

Lusajo Mwaikenda

Kijana kutokea mitaa ya Chamaz Dar es Salaam kazi yake ni kubwa sana kukaba na wakati mwingine kushambulia, ni kati ya wachezaji wachache wanaomudu kucheza eneo lolote la beki kwa usahihi wa hali ya juu akiwa uwanjani ni fahari kumuona mpe muda na macho yako utaona ubora wake, kuanzia mipira ya juu na ya chini pia anavaa jezi ya Azam FC.

 

FABRICE NGOMA

Ni kati ya viungo wachache sana wanaopiga pasi ndefu kwa usahihi wa hali ya juu kwenye kiksoi cha Simba SC amekuwa akitumika zaidi kutuliza eneo la kiungo la timu hiyo kuanzia kupiga pasi na kukba pia.

Impiri Mbombo

Anakipiga kwenye kikosi cha Tabora United ni kati ya mabeki wachache ambao wana takwimu mzuri za kutengeneza pasi “Assist” za magoli mpaka saaa anazo 5 nyuma ya Kipre Junior na Kouassi Attouhoula.

Amekuwa ndiyo silaha ya mashambulizi kwa upande wa pembeni wa kikosi cha Tabora Utd mpe jicho lako awapo kiwanjani maana ni mchezaji wa kuchungwa sana hususa kwenye kutengeneza nafasi za magoli na majukumu mama ya kukaba amekuwa akiyatekeleza kwa usahihi.

 

SOMA ZAIDI : Yanga Fanyeni Kweli Acheni Siasa Za Mpira

1 Comment

  1. Pingback: Kila Nikimuangalia Kibu Denis Namkumbuka Robertinho - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version