Lipo jambo hapa ambalo lazima tulizungumze, kuhusu mchezaji FEISAL SALUM na watu wa Yanga SC naamini wapo baadhi ya Wachambuzi wanamuingiza kwenye chuki bila ya yeye mwenyewe kujua.

Kwanza, YANGA ni taasisi ambayo ni kubwa nchini lakini siyo tu hapa nje ya mipaka yetu kwaiyo siyo rahisi kwa mtu mmoja kuweza kushindana na kundi la watu wote hao.

Kuondoka sehemu huwa haikatazwi lakini ukiendelea kutoa viashiria itaonekana ni kama una chuki na watu hao. Yanga SC ilivyomsajili Fei kutoka Singida hakuwa mchezaji maarufu lakini ukubwa wa Yanga ukampa jina mchezaji huyu na alipendwa sana ndani ya Klabu pale.

Hili la baadhi ya Wachambuzi kukaa kando yake na kuzitumia kalamu zao kama kumtengenezea mafuta na maji siyo kitu kizuri, wapo wenye uelewa kuwa hii ni kawaida lakini wapo wengi akili zao wanazijua mwenyewe, mimi nafikiri wengemuacha Feisal Salum acheze mpira bila ya kumtengenezea chuki kama hizo.

Yuko wapi BERNARD MORRISON ambaye naye alitengenezewa mambo kama hayo baadae ni kama ameuzika mpira wake. Kalamu zinaweza zikawa zinaandika lakini bila ya kutambua zinabomoa kwa kiasi kikubwa sana.

Ushauri wangu kwa FEISAL SALUM Ligi zimemalizika ni muda sasa wa yeye kujitenga na hao ambao ni kama wameamua kuzicheza vita zao na Yanga kupitia mgongo wake kwani asipokuwa makini watamuingiza katika maisha magumu ya soka. TANZANIA yetu wote hii kwaiyo tunatakiwa kuwa makini sana.

SOMA ZAIDI: Azam vs Yanga Tutegemee Fainali Ya Namna Hii Hapa

9 Comments

  1. Slavius nguvumali on

    Fei toto akazane na kazi yake mambo ya kuchanganywa aachane nayo kwasababu ukipenda kufata maneno unaweza kosa mambo mengi kwani yanga Wana kula pesa zake anazo tolea jashi

  2. Feisal anajitengenezea chuki yeye mwenyewe vitendo vyake pale anapokutana na yanga vinazua maswali Kwa mashabiki pia ni kama…. Asilimia kubwa ya mashabiki wa yanga wanatafisiri kama ni kejeli Kwa maboss wake wa Zamani

  3. Yanga pia wanamchukia na kumwonea wivu fei,,, kama co wao kuwa na midomo kama chiriku nadhan fei asingeonesha ishara ya “shut up” nadhan yanga wamuache fei na fei asiwasikilize yanga,,, focus on football zanzibar finest,,,mti wenye matunda ndio hupigwa mawe,,

  4. Mr. Chabhilonda on

    Fei ball player mzuri ila anachotaka kufanya ni kujiona yeye yuko juu kuliko mabingwa(yanga) ushari kwake atimize majukumu yake uwanjani asishindane na taasisi kamz yanga

  5. Mr. Chabhilonda on

    Fei ball player mzuri ila anachotaka kufanya ni kujiona yeye yuko juu kuliko mabingwa(yanga) ushauri kwake atimize majukumu yake uwanjani asishindane na taasisi kamz yanga

  6. Unatoka kweny mwanga unaenda gizan afu unataka watu wakuone 😂🤣😂 fei bhna anway kuna mda makombe yanaihtaji yangu kulko yanga kuhtaji makombe🙏🙏

  7. richylemali386@gmail.com on

    Fei anagecheza mpira na siyo kucheza na wadau wa yanga atapotea Sanaa mtu mmoja huwezi pigana Vita na watu mia.

Leave A Reply


Exit mobile version