Michuano ya kombe la mataifa barani Afrika kwa mwaka2023 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi January 12 nchini Ivory Coast huku mataifa 24 yaliyofuzu yakishiriki katika mashindano hayo.

Kwa msimu wa mwaka 2023 timu za mataifa zilizofuzu ni Pamoja na Ivory Coat ambaye ni mwenyeji wa michuano hiyo lakini pia na Nigeria, Equatorial Guinea, Guinea-Bissau, Misri, Ghana, Cape Verde, Msumbiji, Senegal, Cameroon, Guinea, The Gambia, Algeria, Burkina Faso, Mauritania, Angola, Tunisia, Mali, Afrika Kusini, Namibia, Morocco, DR Congo, Zambia Pamoja na Tanzania.

Katika msimu huu viwanja sita vittumika kutoka katika miji mitano tofauti huku viwili vikiwa katika mji mkuu wa Ivory Coast , Abdijan. Na viwanja hivyo ni hivi vifuatavyo:

Uwanja wa Alassane Outtara , Abdijan 

Huu ni uwanja wenye uwezo wa kumudu mashabiki elfu sitini (60,000) na ulifunguliwa mwaka 2020 na ndio uwanja mkubwa zaidi nchini Ivory Coast. Zamani ulikua unafahamika kama uwanja wa taifa la Ivory Coast kabla ya kubadilishwa na kupewa jina la Allasane Outarra.

Uwanja wa Stade National de la Côte d’Ivoire (2020–2023) huu una uwezo wa kumudu mashabiki elfu thelathini na tatu ( 33,000) na unapatikana katika jiji ;a Abdijan.

Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)

Stade de la Paix, Bouake (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 40,000)

Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Korhogo (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)

Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro (wenye uwezo wa kumudu mashabiki 20,000)

Viwanja vyote aidha ni vipya au vimefanyiwa ukarabati kabla ya Afcon, huku serikali ikitumia dola za kimarekani bilioni moja katika miradi ya miundombinu kote nchini.

Mashindano hayo awali yalipangwa kufanyika Juni-Julai 2023, lakini yalisogezwa ili kuepuka mgongano na msimu wa mvua wa Afrika Magharibi.

Endelea kusoma zaidi kuhusu michuano ya mataifa bara la Africa (AFCON 2023) kwa kugusa hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version