Kwa Tanzania utakua ni mchezo ambao utafuatiliwa kwa kina kabisa kwa mashabiki wa Simba lakini pia na wapenda mpira kutoka hapa nchini mchezo wa makundi ligi ya mabingwa Afrika kati ya Asec Mimosas kutoka nchini Ivory Coast dhidi ya Simba Sc Tanzania.

Ukiutazama kwa kawaida kabisa unaonekana mchezo mgumu kutokana na jinsi ambavyo Asec wamekua na balaa zito katika michuano ya kimataifa msimu huu lakini pia na mwendelezo wa kawaida wa klabu ya Simba wakiwa bado wanaendelea kujitafuta.

Kuna huu mpambano wa Abdelhak Benchikha ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya Simba na Julien Chevalier ambaye ni kocha wa ASEC makocha wawili ambao wanatumia mifumo / miundo tofauti lakini wote wanatumia mabeki wanne nyuma,

ASEC Mimosas 4-4-2

Simba Sc: 4-2-3-1

Walinzi wanne nyuma: wanafanana

Viungo wanne katikati : hawafanani

Washambuliaji wawili juu: hawafanani

Tuangalie jinsi wanavyotumia hii mifumo / miundo : tofauti ipo kuanzia build up, pressing na matumizi ya wingback zao

1: Pressing:

ASEC Mimosas wanapenda kukabia juu zaidi kabla ya kushuka katikati na sio nyuma kabisa, kazi inayoanza kufanywa na Mofossé na Pokou: Wakati Simba wao huwa wanapenda kuanzia kuzuia katikati ya kiwanja na sio juu zaidi ambapo kazi inaanza kufanywa na Kibu na Mzamiru

2: Wingbacks:

ASEC Mimosas wao wingbacks zao huanzia nyuma kabisa na kufika juu haraka pamoja na viungo wao, kwa maana yake wanafika kwa urahisi na inakuwa rahisi kushambulia nafasi zinazokua wazi. Simba wao wingbacks zao mara nyingi huanzia kujipanga vizuri kuanzia juu kama mawinga haswa pale timu ikiwa na mpira ili kuongeza idadi ya washambuliaji kwa haraka.

3: Build up

Hapa ndipo huwa wanafanana ASEC Mimosas na Simba kwa kuanza na pasi fupi fupi za nyuma kadhaa kabla ya kupiga pasi za mbele hasa kwa namba 10 na 8 wao wanaokuwa kwenye halfspaces na fullspaces

 

ASEC Mimosas vs Simba, itakuwa game nzuri sana na nina ushauri kwa Simba kuwa kuna ukubwa wa timu na uzito wa mechi , Mechi yoyote haijalishi unacheza na nani haiwezi kuwa mechi nyepesi na wepesi wa mechi ni jinsi gani wewe unavyotekeleza maelekezo ya Kocha na group zima la timu kwa uzuri ndipo mechi inaonekana nyepesi.

SOMA ZAIDI: Kwa Hili Ayoub Kaitia Matatani Simba Kimataifa?

1 Comment

  1. Pingback: Asec vs Simba Sio Mechi Ya Kawaida , Ni Vita Ngumu Sana - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version