Viongozi wa Simba wanajiroga wenyewe na kujitega kwenye mtego mbaya kwa mashabiki wao kwani ukitazama tu mtiririko wa namna ambavyo kumekua na mabadiliko ya makocha ndani ya klabu hiyo inaonesha kuwa kuna shida mahali ambayo inawafanya mashabiki kutokua na imani na viongozi wao.

Kama ulikua hufahamu ni kuwa Simba wameendelea kuachana na makocha wao kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na katika miaka hiyo 3 imekua katika mtiririko huu hapa :

 

Novemba 2021 – Mei 2022

Pablo Franco

 

Juni 2022 – Septemba 2022

Zoran Mac

 

Septemba 2022 – Januari 2023

Juma Mgunda

 

Januari 2023 – Novemba 2023

Roberto ‘Robertinho’ Olivieira

 

Novemba 2023 – Aprili 2024

Abdelhak Benchikha

 

Hii inashiria kwamba kuna shida ndani ya uongozi wa Simba na shida kubwa kuna presha ya kutaka kuendelea kupata mafanikio ambayo waliyapata kwa kipindi cha misimu minne mfululizo lakini hadi sasa kumekuwa na kuyumba kwa mafanikio hayo ambayo yanapelekea hata makocha kufukuzwa au makocha kuvunja mkataba na klabu hiyo

Lakini pia ukitazama ishu ya kuondoka kwa Benchikha si ishu ya mojakwa moja ya matatizo ya kifamilia bali inaonyesha ni makubwa wanayaoyataka Simba lakini hayaendani na uwekezaji waliouweka kwa msimu huu,ikiwemo wachezaji ambao walikuwepo Simba kwa sasa ilikuwa inamuonyesha kocha anawakati mgumu zaidi kufikia kile Simba sc wanachokitaka na ukizingatia hali ya muendelezo wa matokeo yaliyopo licha ya kubeba kombe la Muungano.

Uongozi wa Simba unapaswa kufahamu kuwa mpira kuna kipindi unaweza ukapitia kwenye wakati mgumu na kwenda nje kabisa ya malengo yao lakini nafasi ipo kwao kujipanga vizuri na kila mmoja atimize majukumu yake bila kuingilia majukumu ya mtu mwingine anaye husika katika usajili wamuache afanye usajili ulio sahihi kwa tafsiri ya kocha ndiye awe na jukumu hilo kwa kushirikiana na skauti aliyekuwepo klabuni hapo .

Pia watafute kocha mkuu mapema kabla msimu haujaisha ili apate nafasi ya kuchunguza timu na kuanza kusuka timu ambayo italeta ushindani mkubwa zaidi kwenye mashindano yote ikiwemo ile ya kimataifa.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa:

1.Je wanaohusika kufukuza na kuajiri makocha simba kwenye misimu yote hiyo si ndiyo hao hao viongozi wapo je wao hawana matatizo? Mbona hawawajibiki.

2.Kama kubadili makocha kuna tija mbona kuleta mataji ya ubingwa hatuyaaoni.?

SOMA ZAIDI: Waraka Mzito Wa Hamisi Kigwangalla Kuhusu “Kuinunua Simba”

19 Comments

  1. Viongozi wa club pia na wao wajitazame maana wanaweza wakawa wanalaumu makocha kumbe wao ndio tatizo kubwa linalofanya timu iendelee kuwa katika mtiririko mbaya

  2. Msimu ujao Simba atashuka daraja Kama hawataacha hii Tabia ya kuwafanya makocha kuwa wanakimbia kimbia Hali ndo kwanza inaenda kuwa mbaya zaidi.

    TAJIRI ABAAAS.

  3. Shida sio makocha , shida inaanza kwa viongozi wetu ila nngependa kutoa ushaur kwamb team iwee inamilikiwa na rais na sio kam ilvyo kila mtu aweke hisa zake, achaguliwe mwenye kiti afu aje kutupiga , uhalisia ni kwamb kweny mpira na kupanda na kushuka ila sisi tunashushwa na viongozi wetu wenyew…..

  4. Tunangoja msimu Uishe ,alafu waone nguvu ya mashabiki ,tusipoenda kuwatoa wenyewe huko maofisini…🤯🤯🤯#simbanguvumoja

  5. Kosa la Simba haijui muda sahihi WA kuachana na mchezaji katika wakati sahihi regardless umuhimu wake ukoje… Mfano juzikati Yanga imeachana na Jesus moloko, kabla waliachana na djuma shabani , yaniq bangala, Feisal Salim ambao wote Bado ukiwaangalia ni kama Wana umuhimu kwenye club,, 🤬🤬🤬🤬. Naomba kuwasilisha ✍🏿

  6. Huu ni mfumo wa ulaji nazani Kwa viongoz wa Simba ndio maana timu haifanyi vizur. Hii timu mwekezaji angekabiziwa timu tu

  7. Daaah sema mashabiki wa Simba huwa wanafurahisha yani wanachekesha sana, leo Mchezaj X ata perform vibaya au tim nzima itapata matokeo mabaya…then after game mashabiki watalalamika sana watausema uongozi ufukuze wchezaji ila utashangaa next game wakishinda ata goli moja wanasahau yote utaskia ohh dhambi za Mchezaj X nipewe mimi Mara Fundi wa magoli cha ajabu wakifungwa tena lawama kama mwanzo
    😀😀😀

  8. Viongozi wapnguzwe na timu bora abaki nayo mgunda awe kocha mkuu basii.
    Na wachezaji wazee wote wapunguzwe
    Akianzwa na saido

  9. Asilimia kubwa ya timu zetu hizi kubwa azisajiri zinaokoteza wachezaji yanga kwa misimu hii mitatu kaokota supa ila simba kajiokotea magarasa yote ila utafika msimu simba simba kuokota supa naye ataludi kwenye fomu

  10. Basically, Simba ni timu nzuri lakini Ina minimum mibovu hapa karibuni shida ya kwanza ni uongozi wa simba unashindwa kufanya maamuzi kwa usahihi mfano kwenye ishu ya scouting. Cha pili ni kwamba simba nzima imeshindwa kuelewa namna kiwanda cha mpira kinavoendeshwa..Profesional football ni lazima UMPE KOCHA MUDA WAKUTOSHA ASUKE TIMU KUTOKANA NA FALSAFA ZAKE NA ANUNUE WACHEZAJI ANAO WATAKA YEYE SIO MASHABIKI WANAVOTAKA. MFANO MZURI JURGEN KLOPP ALIVOTUA LIVERPOOL ILIMCHUKUA MIAKA MI4 KUTWAA KOMBE LAKE LA KWANZA.
    NI MUDA WA SIMBA KUBADILI MFUMO MZIMA WA KUENDESHA TIMU

  11. Kipengele ambacho Simba imezingua ni kwenye ishu ya CEO na scouting..Babra Gonzalez alikuwa anajitahidi sana kuongoza club vizur ila saiz sijui inakuwaje pale Msimbazii…Linganisha scouting ya Simba na Yanga…Yanga yuko Miles nyingi away from Simba…

  12. Mlivyokuwa na hasira wanathimba utadhani siyo nyie mliochukua kombe la muungano! Hongereni watani,,, fukuza wote hadi akili iwakae sawa,,,,,, YANGA BINGWA!

  13. Pingback: KOTI JEUSI ( Sehemu Ya Kwanza) KOTI JEUSI - 01 - Kijiweni

  14. Viongozi wa simba tunaomba mjiuzuru kwa kurinda heshima yenu na kwa faida ya tumu kiujumla, nyinyi sio viongozi wa mpila, Sawa tunajua hakuna timu isiyopitia wakati mgumu lakini kwa timu kubwa kama SIMBA haitakiwi kusota na matokeo mabovu kwa zaidi ya misimu miwili hadi mitatu na sasa ni wazi kabisa kuwa tutaenderea hivi kwa msimu wa nne, HII NI BARUA YA WAZI KWENU VIONGOZI kama kweri ni wapenzi wa simba basi mnatakiwa kuchukua maamuzi magumu na kuwapa wengine dhamana ya kuiongoza SIMBA. Benchika ni kocha mwenye CV kubwa  sana kama dirisha dogo mngempatia wachezaji aliowataka  huwenda leo hii asingeondoka na kuvumilia dirisha kubwa aboreshe tena timu, wachezaji waliopo saizi sio kwamba ni wabovu au hawana viwango la hasha ila simba kwa sasa inahitaji wachezaji wenye status kubwa zaizi ya hawa wa sasa, lawama ata sio kwa  wachezaji wala kwa kocha lawama ni  kwenu viongozi mlioshindwa kwenda na wakati na kujua football ya sasa inataka nini. Mfano, hauwezi kumuacha mchezaji kama Baleke na Phili nakumleta Jobe na Fredi ambao hata haiitaji kuwa na taaluma ya ukocha unaona kabisa wapo chini ya uwezo wa Baleke na Phiri na bado mmekuwa mkibolonga kwa wachezaji wengi tuh. Tafadharini sana tunawapenda na tunashukuru kwa kile mlichotupatia saizi wapeni nafasi wengine tena😢🙏 KUJIUZURU SIO ZAMBI NI KUJITUNZIA HESHIMA KAMA ALIVYOFANYA KOCHA BONCHIKA.

  15. Pingback: Mashujaa vs Yanga Tutegemee Mchezo Wa Aina Gani? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version