Mshambulizi wa Real Madrid Vinicius Junior amekataa jezi namba 7 ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ameripotiwa kupewa jezi ya msimu wa 2023-24 lakini hana nia ya kuvaa jezi hiyo ya kifahari.
Mbrazil huyo anavaa jezi namba 20 kwa Los Blancos huku mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard kwa sasa akishikilia nambari 7.
ESPN Brazil inaripoti kuwa Madrid wako tayari kukabidhi jezi namba 7 kwa Vinicius, lakini nyota huyo wa Kombe la Dunia alikataa kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo, Raul, Amancio, Raymond Kopa, Juanito na Emilio Butragueno.
Vinicius alijiunga na Real Madrid mwaka wa 2018 kwa ada ya Euro milioni 45 na alipewa nambari 20, akisema kuwa hiyo ni nambari yake anayopendelea na imemletea bahati katika kazi yake.
Ikiwa Vinicius atapewa jezi namba 7 msimu ujao, inamaanisha kuondolewa kwa Eden Hazard katika klabu hiyo.