Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa wamepokea mashine za VAR zitakazotumika kuratibu soka la Tanzania Bara kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Karia ameyasema hayo mbele ya wajumbe walioshiriki katika mkutano mkuu wa mwaka wa 18 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania uliofanyika mkoani Iringa na kusisitiza kuwa ni mafanikio makubwa kwani uwepo wa VAR zitasaidia kuleta ufanisi wa uamuzi wa matokeo wakati wa michezo na kuondoa malalamiko ambayo hujitokeza mara kwa mara.

Katika hatua nyingine, Rais Karia amesema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeipatia Tanzania mipira ya viwango vya kimataifa 10,000 ambayo itagawiwa kwa timu mbalimbali nchini huku akisema kuwa hatua hiyo ni kutokana na mafanikio ambayo Tanzania imepata ikiwa ni pamoja Twiga Stars kufuzu WAFCON, ikiwa ni nchi pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kufikia hatua hiyo na Taifa Stars kufuzu AFCON.

Katika mkutano huo wa mwaka, Hersi Said ambaye ni Rais wa klabu ya Yanga ameteuliwa na Rais Karia kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya AFCON na CHAN nchini Tanzania.

Endelea kusoma habari za Ligi kuu kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version