Serikali ya Tanzania imeingia mkataba na kampuni ya ukandarasi kutoka China kukarabati uwanja wa Uhuru uliopo Dar es salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 19.7.

Ukarabati wa uwanja huo utatumia miezi 12 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika #AFCON2027

Mdau Wa KIJIWENI unatamani maeneo gani yafanyiwe marekebisho makubwa zaidi kwa gharama hizo ambazo zimetajwa za kuukarabati uwanja huu?

CHANGIA MADA HII PIA: Mchezaji Gani Wa Nje Hapa Ligi Kuu Amekuwa Bora Zaidi Kwako?

17 Comments

    • Rashidy samweli on

      Pitch na majukwaa afu mamb ya kapet kizaman hyo wenzetu wameachaga hzo bhna sema nn uwanja wa uhuru sjawah ukubali😁

  1. Unahitaji maboresho Sana hususani pale kwenye jukwaa la mashabiki,, inabidi kuwapo kwa eneo kubwa kwa mashabiki pia katika eneo la bench la ufundi. Yote na yote ,lazmza kuboresha taa ,, pitch pamoja na viti .

    • Rashidy samweli on

      Kama mchezaji anatoka yanga kwenda azam unafkir ana malengo ya kwenda mbali huyo? Sametime wachezaji wenyew hawatak kujtuma viwanja vitengenezwe hvo hvo

  2. Astonminer Andaskoo on

    Eneo la pitch na pia eneo la mashabiki wajaribu kufanya ukarabati uwanja uwe level ya New Amaan Complex

  3. Ally Mwamlongo on

    Kiufupi uwanja wa uhuru sio wa kisasa, ulihitaji marekebisho makubwa mno. Kuanzia kwenye pitch, majukwaa, vyooni dressing room na ikiwezekana uwekwe hadi taa

  4. Daniel cupa official on

    Waweke VAR na cam za azam humohumo tuone wanavyo fanya kazi yasije yale ya masandawana goli lina ingia VAR inakataa … Inaonekana wanajalidiligi humo ndani kutoa video za uongo…. tunataka tuwaone wanavyo fanya kazi zao

  5. Pingback: Akiondoka Benchika , Tutegemee Simba Gani Msimu Ujao? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version