Saido akiwa Yanga iliishi maisha yenye furaha muda wote, aliheshimika na kuimbwa Kwa melodi tamu zisizomchosha masikio, melodi zilizoisindikizwa na nickname ya “godfather wa Bujumbura”,  akiwa Simba imekuwa kinyume kabisa, haheshimiki na hakubaliki licha ya kuwa yeye ndiye top score wa misimu miwili yote mfululizo, anaitwa majina ya kila namna kama ishara ya kubeza mchango wake ndani ya timu.

Baada ya usajili wake kukamilika na kujiunga na timu pale Mwanza CCM kirumba akitokea Geita, alitoa kauli za kuwananga waajiri wake wa zamani Yanga huku akijipambanua kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Simba yeye na familia yake ambayo nayo ikathibitisha Saido ni Simba, Kuna muda alijiingiza kwenye sakata la Feisal Salum akimwaminisha kama anahitaji Mafanikio aondoke Yanga aende Simba.

Waswahili husema usinene ukamala, Baada ya misimu miwili Saido amechapisha ujumbe katika kurasa zake za mitandao ya kijamii akisema

“Mtu mkubwa haadhibiwi kwa kuchapwa fimbo bali adhabu ya mtu mzima ni kuwa sehemu isio sahihi kwake na hakika nimejifunza.”

Aidha ishara anazozitoa Kwa Sasa (Kuwaziba midomo) Kila akifunga nazo ni lugha tosha kabisa kuwa kifuani mwake katunza nini kinamsibu.

Hili ni funzo kwa Wachezaji wanaochipukia katika kuheshimu kazi yake na waajiri wao wa zamani na wasasa,,,,, Dunia duara na kesho ni fumbo.

SOMA ZAIDI: Tumsubiri Kramo Au Ni Wakati Wa Kutafuta Mchezaji Mwingine?

5 Comments

  1. unajua bongo bwana ndio nchi pekee inayoweza kukufanfa ukawa super star na ndio nchi pekee inatoweza kukuangusha kwa wakat mfupi sana na watu wengi wa kigen bado hawajalitambua hilo hivyo bhas wakae kwa kutulia.

  2. Anthony jaden on

    Anaeza kuwa na mapenzi ya dhati na simba ila kaja wakati mbaya ambapo team haina mwendelezo bora, hata yeye Gari imekata kilometer inatosha Sasa anaeweza kuwa kama yule wa kagera(chirwa) hata yeye aliimbwa nao kaamua kumaliza uzee hapo, kifupi simba walibugi kumsajili saidio, team ina
    Boko-30+
    Nyoni-30+
    Chama30+
    Kapombe30+
    Kenedy30+
    Mzamiru30+
    Inonga30+ alafu unatak ubingwa, mmmh

  3. Wachezaji wengine wajifunze jambo hapa kwa saido, pindi wanapotoka kwenda upande mwingine wasizarau upande wanaotoka na kuamini kwamba huko aelekeako kutakuwa Bora zaidi au yeye yupo sahihi zaidi hivo kuwabeza waajili wake wa zamani, siku hazilingani wasifikiri kuwa siku zote watakuwa wapo kwenye viwango Bora vile vile, so chamsingi wajifunze ku-behave ili baadae isiharibu status na sifa zao.

  4. Pingback: Je Simba Wana Mradi Mpya Au Wanataka Kurudisha Wa Zamani?

Leave A Reply


Exit mobile version