Nimekuwa mkosoaji mkubwa wa Shirikisho la soka la Tanzania kutokana na sababu za waamuzi na mambo mengine mengi ambayo siwezi yasema yote lakini mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Karia amefanya na ziada kwenye mpira wetu. Amevunja rekodi nyingi kwenye tasnia ya mpira ambazo hazitaki maelezo mengi kuyataja.

Kwakuwa amefanya na ziada basi na wadau wa mpira tumtendee na yeye cha ziada. Tumpe muda zaidi aweze kuikamilisha ndoto yake ya kuiandaa AFCON 2027. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Karia ndo Rais bora zaid wa TFF kuwahi kutokea, ubora unapimwa na mafanikio, hakuna Rais wa TFF anayefikia mafanikio ya Karia.

Kuanzia thamani ya ligi kwasasa, mafanikio ya Vilabu na Timu za Taifa katika mashindano mbalimbali, hapa nazungumzia timu za Taifa zote, vijana, wanawake, walemavu na hii Taifa Stars, Ushabiki wa soka katika nchi umekua sana, thamani na maslahi ya wachezaji hasa wazawa ambao walikuwa hawana thamanI, miundombinu kama viwanja na kadhalika.

Mapungufu hayakosekani, lakini huyu mzee ana mazuri mengi kuliko mapungufu, apewe maua yake kwa jinsi ambavyo tumeona mabadiliko makubwa ambayo ameyafanya licha ya kwamba kuna muda kunakua na changamoto lakini ni vyema tukachukua kuwa njia mojawapo ya kujifunza kwa wakati mwingine haswa pale atakapochaguliwa Rais mwingine wa TFF.

SOMA ZAIDI: Kama Ni Ufalme Wa Mbinguni, Chama Ameubeba Wa Duniani

 

Leave A Reply


Exit mobile version