Michuano ya AFCON 2023 inaendelea kushika kasi na hii leo kuna michezo kadhaa ambayo itachezwa na bila shaka wawekezaji wako makini kabisa kuandaa mikeka yao ya ushindi katika mechi hizi ambazo ni mechi za mapema za saa 2 usiku ambapo Guinea Bissau vs Nigeria lakini pia mechi ya Equatorial Guinea vs Ivory Coast na zile mechi za saa 5 usiku ambapo Mozambique vs Ghana huku Cape Verde vs Egypt.

Hizi ni mechi za kusisimua zenye ushindani mkubwa kati ya timu bora za mpira wa miguu barani Afrika na namna ambavyo makundi yao yalivyo ni wazi ikawa sababu ya wao wote kucheza muda mmoja ili kepuka kupanga matokeo.

Katika kipindi hiki, wengi hujaribu kubashiri matokeo ya ushindi wa moja kwa moja katika michuano hii ambayo imekua na matokeo ya kushangaza haswa kwa timu ambazo hazikutegemewa kabisa. Hata hivyo,nina sababu kadhaa za kukueleza kwanini michezo ya leo siyo ya kutabiri ushindi wa moja kwa moja kwa baadhi ya timu ambazo unaziona kuwa na majina

Katika mechi za leo timu zote zinapambania kufuzu lakini pia zipo ambazo zimekwishafuzu Kwenda hatua ya 16 bora hivyo hakuna hakikisho la ushindi wa moja kwa moja. Timu zenye viwango vya juu zinaweza kushindwa na timu zinazochukuliwa kuwa dhaifu.

Kumekua na mambo mengi ya kushtukiza kama vile kadi nyekundu, majeraha ya ghafla, au hata kupatikana kwa penati ambazo hazikutarajiwa jambo ambalo linaweza kuathiri matokeo ya moja kwa moja, na hivyo, kutobashiri ushindi wa moja kwa moja kunaweza kutoa uhuru zaidi.

Kwenye michuano ya AFCON ya mwaka huu kumekua na michezo ambayo timu zinazochukuliwa kuwa dhaifu zinaweza kucheza vizuri na kutoa upinzani mkali kwa timu zenye viwango vya juu. Hii inasababisha kupelekea kutokea kwa matokeo usiyoyatarajia ni wazi kuwa unaweza kutoa fursa zaidi za kuchagua matokeo, kama vile kuwepo kwa magoli chini ya 4 lakini pia kubetia hat timu kubwa kupata walau goli 1.

Unaweza kuzingatia takwimu na historia ya timu japokua sio mechi zote katika michuano ya AFCON mwaka huu imejibeba kwa takwimu zaidi ya Senegal.

Kwa kuzingatia mambo haya, wengi wanaweza kuchagua kutobashiri ushindi wa moja kwa moja na badala yake kutafuta chaguzi zingine kama vile droo, idadi ya magoli, au matokeo mengine yanayohusiana na mchezo. Hata hivyo, katika mpira wa miguu, hakuna njia kamili ya ubashiri, na kila mchezo unaweza kuwa tofauti.

SOMA ZAIDI: AFCON 2027 Sio Mbali Tumejiandaaje Kwenye Viwanja?

1 Comment

  1. Pingback: Huu Hapa Mkeka Wa Kumpiga Mhindi Leo - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version