Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amemsifu Todd Boehly kwa kumfuta kazi Graham Potter, akisema amefanya uamuzi sahihi.
Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na kushindwa 2-0 na Aston Villa hivi karibuni katika uwanja wa Stamford Bridge, Todd Boehly aliamua kumfuta kazi Potter.
Potter aliiongoza timu hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi 12 kati ya 31 akiwa kocha wa Blues.
Akiongea kwenye Sky Sports, Carragher, mchezaji wa zamani wa Premier League, amesema uhusiano kati ya Chelsea na Potter haukuweza kufanya kazi.
Alisema sababu halisi ya kumfuta kazi Potter ni kwamba mashabiki wa klabu hiyo wamezoea kushinda mataji kwa miaka 20 iliyopita.
Aliongeza kuwa pia wamezoea kubadilisha makocha na kuwaajiri makocha ambao wameshinda Ligi ya Mabingwa.
“Kwa hivyo wanaimba kwa Graham Potter ‘Hujui unachofanya!’ Hiyo ni sababu moja ya yeye kuondoka.
“Uteuzi ulikuwa mbaya tangu mwanzo. Nimekuwa mkali sana kwa Todd Boehly lakini nadhani hii ni uamuzi wa kwanza ambao amefanya sahihi,” alisema