Moja kati ya mechi ambayo bila shaka watu wengi kwa maoni yao walitamani iwe ndio fainali yenyewe ni mchezo wa AFCON  uliowakutanisha Nigeria dhidi ya Afrika Kusini moja kati ya mechi bora sana iliyochezwa ya nusu fainali kutokana na matukio ambayo yalijitokeza katika mchezo huo.

Ukiizungumzia nusu fainali hii basi kuna majina ambayo huwezi kuyaacha kuyataja ambayo katika nusu fainali hii walikua na balaa kubwa sana na hapa tumekuandalia majina haya matatu ambayo yalionesha mambo ya kushtukiza sana.

Stanley Nwabali:

Huyu unaweza kusema katika hatua ya nusu fainali ndio shujaa wa Nigeria kwenye toleo la 34 la AFCON aliyezaliwa kwenye kijiji cha River’s state kwenye jamii ya Okwuzi miaka 27 iliyopita akiwa na urefu wa futi 6.

Nwabali anaitumikia klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini na kwenye hatua ya nusu fainali alikuwa na kiwango bora sana dhidi ya Afrika Kusini nchi ambayo sehemu kubwa ya kusakata kwake kabumbu anafanyia kazi huko.

Kwenye mchezo huo alicheza Dakika 120 akiwa ndiyo Mchezaji bora wa mechi kwani alifanya save 7 za hatari huku akipiga pasi 24 na 12 kati ya hizo zikifika kwa usahihi, pia alipiga pasi 17 ndefu na 5 zikifika kwa wahusika, akiokoa mipira ya juu (Punches) mara 3, akifanya recover mara 13.

Mchezo huo ulikwenda hadi kwenye hatua ya mikwaju ya penalti na kipa huyu alifanikiwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti, mkwaju wa kwanza kwa upande wa Afrika Kusini uliyopigwa na Teboho Mokoena aliokoa pamoja na penalti ya mshambuliaji Evidence Makgopa.

Nwabali amefanikiwa kucheza michezo yote ya AFCON kwa upande wa Nigeria kuanzia hatua ya Makundi na kabla ya mchezo wa nusu fainali alicheza mechi 6 bila kuruhusu goli lolote lile.

 

Teboho Mokoena:

Kiungo wa Bafana Bafana mzaliwa wa eneo la Bethlehem ya Afrika Kusini akiwa na Futi 5 na umri wa miaka 27 akiwatumikia miamba ya African Football League, Mamelod Sundowns ya nyumbani kwao Afrika Kusini.

Teboho Mokoena alikuwa na kiwango bora sana kwenye mchezo wa hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Nigeria na alikuwa mchezaji wa pili kwa kuwa na nyota 8.1 nyuma ya kipa Stanley Nwabali ambaye alikuwa na 8.3.

Alicheza dakika 120 akifanikiwa kufunga goli moja kwa mkwaju wa penalti, alipiga pasi 84 na pasi 70 zilifika kwa usahihi, akitengeneza nafasi moja na akipiga mashuti mawili “On target” akiwa kwenye eneo la kushambulia aligusa mipira mara 99 na alipiga pasi 15 kwenye eneo la mwisho la mpinzani “Final third” huku akifanikiwa kupiga kupiga krosi 3 na moja tu ndiyo ilifanikiwa kufika huku akipiga pasi ndefu 9 na 5 zikafika pamoja na kona moja.

Nje ya kusaidia mashambulizi Teboho Mokoena alifanikiwa kusaidia ulinzi kwa kufanya clearance moja na “Recover” mara 7.

Ronwen Williams

Ukiizungumzia timu ya taifa ya Afrika Kusini kwenye michuano ya mataifa barani Afrika haswa hatua ya Robo Fainali huwezi kuacha kumtaja kapteni wa timu hiyo ambaye ni golikipa Ronwen Williams mzaliwa wa Port Elizabeth kwenye jamii ya Gelvandale eneo la Gqeberha mwenye umri wa miaka 32 ambaye pia ni kipa wa klabu ya Mamelod Sundowns.

Alikuwa mchezaji wa tatu aliyekuwa na kiwango bora na nyota 8.0 nyuma ya Stanley Nwabali na Teboho Mokoena kwenye mchezo wa nusu fainali.

Amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Afrika Kusini na nusu fainali alicheza dakika 120 akifanikiwa kufanya save 9, akirusha mipira 5, pia alipiga mipira 12 mirefu na kati ya hiyo mipira 5 tu ilifika kwa wahusika na kufanya “Recover” mara 10.

SOMA ZAIDI: Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika

1 Comment

  1. Pingback: Afrika Kusini vs DR Congo Wachezaji Hawa Ni Balaa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version