Wakati michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) ikianza mitazamo ya wengi ilikuwa ni ngumu kuamini mchezaji kutoka Ligi kuu ya NBC kufanya vizuri na kuonyesha thamani ya Ligi yetu kwa sasa ni licha ya Ligi yetu kuanza kufanya vizuri kwa vilabu vyetu kupata matokeo mazuri kwenye michuano ya kimataifa kuanzia kombe la shirikisho na hata klabu bingwa barani Afrika.

Kwa sasa ni ngumu mchezaji kutoka Afrika Mashariki na kati na hata Magharibi mwa Tanzania kukataa ofa ya klabu yoyote ile hususa klabu za Simba, Yanga na Azam FC kutokana na kuwa michuano hii imeendelea kuonyesha thamani ya Ligi yetu na hiyo ni kutokana na wachezaji wachache kutoka NBC PL kushiriki michuano hiyo na kuonyesha kiwango bora na chenye muendelezo kuanzia mchezo wa kwanza wa makundi hadi wa mwisho uliyotamatika January 25,2024.

Hii leo tutazame wachezaji ambao wameonesha vviwango vizuri mpaka sasa katika michuano ya AFCON nchini Ivory Coast ambao ni zao la Ligi Kuu ya Nbc ni pamoja na :

1.IBRAHIM HAMAD BACCA 

Huyu ni beki kisiki kutoka Tanzania Visiwani amekuwa na kiwango bora sana kuanzia kwenye klabu yake ya Yanga SC na hata kwenye michuano hii ya AFCON. Licha ya timu yake ya taifa kutolewa ila ardhi ya Raisi Yacine Idriss Diallo ambaye ni makamu wa Raisi wa zamani wa ASEC Mimosas, Ivory Coast na AFAD Djekanou, itaikumbuka miguu ya kijana huyo.

Ibrahim Bacca ameonyesha ubora mkubwa sana kiufundi akiwa bora kwenye mipira ya Juu maarufu kama Aerial Balls, tackling, clearance na hata usahihi wake kwenye kupiga pasi na kuziba makosa madogo yanayojitokeza kwa mabeki wenzake.

2.MOHAMED HUSSEIN “TSHABALALA”

Fahari hii ya Wanasimba kutoka mitaa ya Msimbazi Kariakoo, kabla ya michuano hii kuanza wengi walikuwa wakiamini ni wakati wake kupumzika na kuachia wengine nafasi hiyo kwenye timu ya taifa na klabu yake lakini michuano ya AFCON imekuwa sehemu kwake kudhihirisha ubora wake kuanzia mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi akionyesha ubora mkubwa sana.

Mohamed Hussein maarufu kwa Jina la TSHABALALA au Zimbwe kiufundi alikuwa bora sana kuanzia mchezo wa kwanza akicheza jumla ya dakika 270 sawa na michezo 3, akiwa na ubora wa 78% ya kupiga pasi, usahihi wa kupiga tackling, kuondoa hatari “clearance”, uwezo mzuri wa kuzuia bila kusahau ubora wake wa kukokota mipira. Beki huyu amekuwa na muendelezo mzuri huku akionyesha ubora wake wa kuzuia vizuri pamoja na kushambulia kwa wakati sahihi.

3.NOVATUS DISMAS MIROSHI 

Kitasa hiki kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine akiwa kwa mkopo akitokea Zulte Wergen ya Ubelgiji.Uhodari wake umeonekana akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja kiwanjani ambapo mchezo wa kwanza alicheza kama beki wa pembeni huku mchezo wa mwisho dhidi ya DR Congo akicheza nafasi ya Kiungo mzuiaji.

Novatus Dismas ambaye ni zao la Azam FC amekuwa na kiwango kizuri kwenye michezo yake miwili licha ya kupewa kadi nyekundu dhidi ya Morocco ila uwezo wake umeonekana na kumfanya kuwa sehemu ya Kikosi cha siku cha michezo ya mwisho ya hatua ya makundi AFCON ikihusisha muunganiko wa wachezaji kutoka mataifa 4 tofauti. Ubora wa Novatus kiufundi umeonekana ikiwemo uwezo wake wa kuondoa hatari, kushinda mipira ya juu, uwezo wa kupiga pasi na kukaba kwa usahihi na kusaidia mashambulizi pale ikihitajika.

4.AISHI MANULA “AIR MANULA”

Licha ya kutoka kwenye majeraha ila amekuwa na kiwango kizuri kwenye michuano hii ya AFCON akiwa na muendelezo mzuri wa Performance. Aishi Manula ameonyesha uwezo wake wa kupanga mabeki hususa pale ambapo timu imekuwa ikishambuliwa, ubora wa kuokoa michomo “Saves” 3 dhidi ya DR Congo, akipiga pasi kwa 82% huku akionyesha Uhodari wake kwenye saves za hapo kwa kwapo akiwa kwenye eneo lake “ndani ya box.

5.MBWANA SAMATTA “POPA”

Ndiyo Mchezaji pekee kwenye kikosi cha Taifa stars ambaye ana mafanikio makubwa ngazi ya klabu akiwa na Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika pamoja na Ufungaji bora wa Afrika na Ligi kuu ya Ubelgiji. Samata ameonyesha kiwango bora Licha ya kuwa mshambuliaji ila amekuwa akisaidia kukaba akirudi nyuma kukaba na wakati mwingine kuanzisha mashambulizi kutokea chini.

Mpaka hatua ya makundi imeisha amefanikiwa kucheza dakika 257 sawa na dakika 90 za mchezo mmoja huku michezo  akitolewa dakika ya 80 na 86 ya mchezo. Amekuwa na ubora wa asilimia 77% za usahihi wa pasi zake huku akionyesha uhodari wake kwenye kukokota mpira, kuokoa hatari, na kushinda mipira ya juu.

 

6.BAKARI MWAMNYETO

Kitasa hiki kutokea mitaa ya Jangwani, Kariakoo nyumbani mwa kikosi chake cha Yanga SC amekuwa na kiwango kizuri licha ya wengi kutomzungumzia sana. Mpaka hatua ya makundi inaisha beki huyo amefanikiwa kucheza Dakika 270 sawa na dakika 90 kwa kila mchezo.Mwamnyeto ameonyesha ubora wake hususani kwenye kuokoa mipira ya juu “Aerial duels won”, kupiga pasi, kuokoa Hatari “clearance”.

7.HENOCK INONGA BAKA “VARANE”

Huyu ni Beki wa Simba SC pamoja na kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo. Amecheza Dakika 135 tu sawa na mchezo mmoja akicheza Dakika 90 huku mchezo mmoja akicheza Dakika 45 tu na kuumia.

Licha kupata majeraha ila beki huyo ameonyesha ubora mkubwa sana na kupelekea kujivunia kuwa sehemu ya wachezaji wanaocheza Ligi kuu ya NBC. Baka ameonyesha ubora wake hususani kwenye mipira ya juu, tackling, kupiga pasi kwa usahihi kwa 92%, pamoja na kukaba nafasi vizuri pale mabeki wenzake wanapochelewa kurudi kuzuia.

8.DJIGUI DIARA 

Kipa huyu anayekipiga kwenye kikosi cha “Wananchi” Yanga SC pamoja na kikosi cha Taifa cha Mali.Diara amecheza jumla ya dakika 270 sawa na dakika 90 za michezo yote mitatu ya makundi, akiwa na uwezo wa kupiga pasi, Saves za Hatari pamoja na kuonyesha Uhodari wake wa kufanya recover licha ya kucheza kama kipa. Wachezaji watatu ndiyo ambao wanatoka Ligi kuu ya NBC na timu zao za taifa zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ambao ni Kipa Djigui Diarra wa Mali, Henock Inonga wa DR Congo pamoja na mshambuliaji Stephane Aziz Ki wa Burkina Faso.

9.STEPHANE AZIZ KI 

Kiungo mshambuliaji huyu kutokea mitaa ya Jangwani Kariakoo, Dar es Salaam sehemu ambayo ndiyo makazi ya klabu yake ya Yanga SC.Aziz Ki ndiyo kiungo mshambuliaji wa kigeni pekee anayetokea kwenye Ligi kuu ya NBC anayeshiriki michuano ya AFCON msimu huu akiwa na kikosi chake cha Burkina Faso.

Kiungo huyu amecheza jumla ya dakika 175 tu na amekuwa hodari kwenye kutengeneza nafasi za magoli, kupiga pasi, akiwa na miguso mingi awali kiwanjani.Hata hivyo amekuwa akisaidia eneo la kukaba akiwa eneo Lao la kuzuia na ameonekana ni bora kwenye kuingilia mchezo wa mpinzani.

Mpaka sasa wachezaji watatu ndiyo ambao wanatoka Ligi kuu ya NBC na timu zao za taifa zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ambao ni Kipa Djigui Diarra wa Mali, Henock Inonga wa DR Congo pamoja na mshambuliaji Stephane Aziz Ki wa Burkina Faso.

SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya AFCON Hatua Ya 16 Bora

1 Comment

  1. Pingback: Ule Muda Wa Kufanya Maajabu Kila Kona Umerejea Tanzania - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version