Ukiitazama klabu ya Yanga katika jicho la kishabiki unaweza kuiona namna ambavyo ina balaa inavyokua kiwanjani ambapo kwetu sisi tunaowaangalia katika jicho la namna wanavyotekeleza mifumo ya kocha wao Gamondi pia tunaweza kuitazama kwa namna mbili ambapo tunaingalia katika mifumo yao ambapo ni upande wa ubora na pia katika udhaifu.

Huu hapa uchambuzi mfupi kabisa wa mifumo ya uchezaji wa yanga ambapo kama nilivyosema hapo awali tunaangalia  udhaifu na ubora wao pale wanapokua na mpira lakini pia wanapokua hawana mpira kiwanjani.

Katika mechi za hivi karibuni ambazo ni za maandalizi ya msimu, klabu ya Yanga wameanza na mfumo wa 4-2-3-1 kwenye makaratasi ambapo wachezaji walijipanga hivi :

Yanga walipokuwa na mpira walitaka kuunda muundo ambao ungewafanya wawe na idadi kubwa golini hasa kwa kutumia eneo la kati ambapo Aziz Ki, Dube na Maxi walipanga kuathiri eneo hilo

Lakini muundo wao na mpango wa kutumia eneo la kati haukuwa kama Gamondi alivyotaka kwani ukitazama katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs tumeona jinsi ambavyo Nabi pia ni muumini wa kulitumia sana eneo la kati hivyo kukawa na msongamano eneo la kati ikabidi yanga wamtumie Kibabage kama beki wa kulia anaecheza sana juu ya uwanja kisha wakiwa na mpira Abuya acheze kama Kiungo wa pembeni mshambuliaji (LCM) akisaidiana na Mzize eneo hilo kitendo kilicholazimisha Yanga kucheza muundo huu.

Kisha wakiwa hawana mpira walikuwa na miundo miwili muundo wa kwanza ni 4-1-4-1 muundo wapili ukiwa 4-4-2 ikitegemea katika eneo ambalo Duke Abuya yupo mana mara nyingi alikuwa alicheza pembeni ya aucho lakini kuna mda ilimbidi akabie juu sana ya uwanja

 

Basi huo ndo ulikuwa uchezaji wa yanga

 

Ubora wao ulikuwa huu hapa:

  1. Walikuwa na umbo zuri sana wakiwa hawana mpira kila mchezaji anarudi nyuma kwajili ya kuweka idadi kubwa ya wachezaji kwenye boksi lao
  2. Waliweza sana kumlazimisha kaizer chiefs kutokucheza kwa amani endapo walianza mashambulizi kwenye boksi lao yani kutokea nyuma (Aziz Ki , Dube, Mzize ) na baadhi ya maeneo Duke alikuwa Karibu sana na safu ya ushambuliaji ili kuweka presha kubwa

Udhaifu wa Yanga

  1. Yanga walipoteza sana Mipira ya pili tena kwa hatari zaidi mipira ilikuwa ikizagaa nje ya lango lao wamshukuru mungu kaizer chiefs hawakuwa wakatili leo
  2. Kama ilikuwa ni mbinu ya mchezo sawa muhimu ni matokeo . Lakini wameshindwa kuumiliki mpira hasa kipindi cha pili kuanzia dakika ya 70 Narudia tena kaizer walikuwa wazuri sana leo wapole sana hawakuwa wakatili wamekaa sana na mpira

 

Note: Ni kama Gamondi amebadilisha staili ya uchezaji kutoka msimu jana kuanzia wachezaji anaowategemea

Msimu jana ilikuwa Pacome , Maxi na Aziz lakini sasa hivi nimemuona Max Nzengeli ndio amepewa uhuru afanye lolote uwanjani

SOMA ZAIDI: Barua Kwenu Washambuliaji Kuelekea Msimu Wa 2024/2025

5 Comments

  1. Katika dakika 90 on target za yanga zilikuwa tano wakapata goli nne,ivyo kwenye udhaifu wa pili sikuungi mkono, naamini ni mbinu tu kwamba tuwaache wamiliki mpira alafu tuwafanyie pressing ambazo zilifanya wafanye makosa kwa magoli matatu,ivyo Kaizer kumiliki mpira sio udhaifu bali ni mbinu za mwalimu

  2. Pingback: Bisris Norte Inahitajika  Kwa Timu Zetu Kimataifa

  3. Yanga hawakuwa dhaifu kama ulivyofikiwa wewe kwa upeo wako, hakuna atayokubishia kwa sababu ndivyo ulivyoamini.
    Ila nimwambie kitu yanga walikuwa wanawatengeneza kaizer waingie kwenye mfumo wao yanga,na kaizer iliingia mfumoni wakapigwa 4,usiombee uingie kwenye mfumo wao yanga utaumia.Amini usiamini.kaizer waliingia kwenye mfumo.

Leave A Reply


Exit mobile version