Mechi nzuri iliyoathiriwa na hali ya uwanja kwa kiasi fulani kizuri ni kuwa timu zote zilicheza hapo hapo na level ya uhitaji wa matokeo ilikuwa kubwa yenye kutupa ari kubwa ya wachezaji

Kipindi cha kwanza JKT waliishika mechi vyema mno! Pasi fupi fupi sahihi, pasi ndefu za kumega uwanja, namba nzuri kushambulia lakini makosa yao ni yale yale! Suala la kufunga wao ni gumu kuliko chochote! Hawajashinda tangu Novemba 3, 2023… Wamekosa TOO CLEAR Chances 50 msimu huu!

Yanga walielemewa kipindi cha kwanza kwenye kiungo Aucho alikosa msaada wa Okrah na wenzie… Alijikuta akihangaika na Ndemla na Kapalata lakini bado alionesha uimara. Kipindi cha pili Aziz KI alipotea mchezoni… Mipango mingi ikafia hapo.

Katika mchezo wa leo Hassan Nassor Maulid amecheza vyema sana huku akifahamu wazi kuna ugumu kubattle move nyingi akabaki kulinda madhara ya Aziz KI bila kusogea sana. Yanga waliwakuta walinzi wengi wa JKT muda mwingi kwa sababu yeye alibaki kulinda tu ukuta wake kwa nidhamu kubwa. Ndiye Man of the Match wangu leo

Ibrahim Abdullah Bacca ni complete defender! Anazima miguu yote, juu anaenda, chini yupo… Kipindi cha kwanza yeye alikuwa sababu ya Yanga kuwa salama. Clearance 4 ikiwa double Ni majitoleo makubwa.

Hassan Kapalata kwenye uwanja rough yeye hakuwa tough ila Smart tu Kapasia sana kwenye mapana ya uwanja na hakuwa muoga kufanya maamuzi yake! Anaangushwa sana na safu ya ushambuliaji.

Mchezo wa leo Attohoula Yao wa leo na Majitoleo makubwa… Kuziba njia na energy ya kutosha kupanda na kushuka. Yale maji anayomimina yanaweza kuwa masumbufu ya mabeki wengi tu.

Napenda pasi za kugawa uwanja za Ndemla Kuna muda anafanya mpira uonekane kitu rahisi sana… Akinyanyua tu macho anafanya delivery… So fine and smooth!

Yule Job ni unsung hero. Kibabage anapaswa kujibidiisha haswa kwenye krosi, usahihi wa hesabu zake za kupanda na kushuka. Farid kwa dakika zake chache amemkumbusha kitu.

Mbinu ya JKT kujilinda kipindi cha pili ingeweza kuwazulia msala muda wowote! Walikaribisha mafuriko makubwa na wamefanikiwa kuyazuia kwa beseni

Mamelodi in Mbweni Sassi kawaza sana pale!

FT’ JKT  0 vs 0 Yanga SC

SOMA ZAIDI: Pale Simba Shida Sio Mangungu Ni Wachezaji Hawa

4 Comments

  1. Agripina mwang'onda on

    Uwanja ndo tatizo ikiwezakana ufungiwe kwa ajili ya ukarabati love my team young African hamna baya

Leave A Reply


Exit mobile version