Plan ya Simba SC ilikuwa inafanya kazi vizuri sana hasa bila mpira dhidi ya Wydad .
1: Muundo wa 4-5-1 bila mpira , na kwanini walitumia huu muundo ?
2: Kwasababu unasaidia kuzuia njia kuu mbili za kutengeneza magoli , pembeni na ndani ( Zimbwe na Kapombe ) hawakuachwa wazi sana
3: Funga eneo la katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo yani mbele ya kina Inonga na nyuma ya Ngoma maana yake waliwalazimisha viungo wa Wydad wafanya kazi zao mbele ya kiungo cha Simba kitu ambacho ni faida kwa Simba kwenye kuzuia
4: Box defending : Simba walifanya kazi hii kwa ufanisi katika nyakati nyingi sana ukiacha kwenye goli , Inonga na Malone mipira mingi ya juu ilikuwa yao
✍🏻Nafikiri kilichokosekana kwa Simba ni pale wakiupata mpira kwenda mbele , walikuwa wachache na kufanya mipira mingi ya pili waishinde Wydad na unaelewa kwanini kwasababu kwa kipindi kirefu walikuwa nyuma kwa idadi kubwa ya wachezaji kwahiyo ni ngumu kushambulia kwa wachezaji wengi
✍🏻Wydad walikosa njia za ndani maana yake silaha yao kubwa ilikuwa pembeni ya uwanja kwa kutumia fullbacks wao na wingers wao kwa kutengeneza 2v1 dhidi ya fullbacks wa Simba SC lakini bado hawakuwa na mafanikio makubwa katika maeneo hayo .
✍🏻Wydad wakiwa na 2-1- 4-3 wakiwa na mali lakini wale namba 8 wao wawili walikosa space nyuma ya kiungo cha Simba maana yake wakaanza kukimbia katikati ya mabeki wa kati wa simba na fullbacks wao , sio lazima kupata mpira bali kufungua spaces kwa wingers wao , na bado walikosa kuifungua Simba vizuri mara kwa mara ….. mpaka pale ile faulo iliyowamaliza Simba
NOTE
1: Mpira na ukatili wake wakati unaona unavuna hata alama moja , uki switch off kidogo tu mpira upo wavuni
2: Sio rahisi kuwa Baleke katika muundo huu wa uchezaji maana muda mwingi unakuwa peke yako mbele kukabiliana dhidi ya mabeki wawili na kiungo wa ulinzi sio rahisi
3: Jabrane licha ya kukosa penati , passing game yake , utulivu , ufundi 🔥
4: Bouhra , jinsi anavyo dribble mpira 🔥
5: Simba SC bila mpira wameboresha
6; Draoui , touch ya kwanza , na ule umaliziaji 🔥
7: Ayoub Lakred hali ya kujiamini imerudi na performances nzuri zinaonekana
FT: Wydad 1-0 Simba SC
Unaweza kusoma zaidi habari zetu hapa.