Tuzo za TFF ni Moto..! Ligi kuu Tanzania bara (NBC Premier League) ikiwa imefikia ukingoni Juni 12, 2023 kwa kumalizika Mechi ya fainali ya Azam Sports Federation Cup iliyokutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC na huku ikimalizika katika Viwanja vya Mkwawani Tanga na Yanga SC kuondoka na ubingwa kwa ushindi wa bao 1-0.

Licha ya kuwakosa Wachezaji wao muhimu katika kikosi ambao ni Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki waliotimkia kutumikia mechi za kimataifa, Bao pekee la ushindi la Yanga SC liliwekwa kambani na Mshambuliaji Kennedy  Musonda dakika ya 13 na kuwafanya wana jangwani hao kutetea tena ubingwa wao msimu huu.

Baada ya kumalizika kwa michuano hiyo na Ligi kiujumla, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitamatisha kwa kutolewa kwa Tuzo katika msimu huu wa 2022/2023 zilizofanyika katika Viwanja wa ufundi vya TFF katika vipengele mbalimbali katika soka nchini Tanzania zilizofanyika hapo mkoani Tanga na vigogo mbalimbali wakiondoka na Tuzo usiku huo.

Hizi hapa ni  baadhi ya Tuzo ambazo ziligonga vichwa vya mashabiki wa soka kutokana na ukubwa wake na hawa ndio washindi waliozinyakua:

  1. Mchezaji bora Umri miaka 20 ni Clement Mzize kutoka Yanga SC
  2. Mchezaji bora 1st League ni Tungu R. Kachinje kutoka Stand United FC
  3. Mchezaji bora ligi ya Championship ni Edward Songo kutoka JKT Tanzania
  4. Timu yenye nidhamu ligi kuu ya wanawake (SWPL) ni Alliance Girls
  5. Mcheaji bora chipukizi Ligi ya wanawake (SWPL) ni Winfrida Charles kutoka Alliance Girls
  6. Golikipa bora Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara (SWPL) ni Naitath Abbass kutoka JKT Queens
  7. Muamuzi bora Ligi kuu Tanzania bara ni Jonesya Rukya
  8. Mfungaji bora Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara (SWPL) ni  Janeth Shikangwa kutoka Simba Queens
  9. Kipengele cha Kocha bora ligi kuu ya wanawake (SWPL) ni Ally Ally kutoka JKT Queens
  10. Mchezaji bora wa ligi kuu ya wanawake (SWPL) ni Donisia Minja kutoka JKT Queens
  11. Tuzo ya heshima kwenye soka la wanawake nchini Tanzania imekwenda kwa Angela Bilal
  12. Mchezaji Gwiji wa Zamani ni Leopold Taso aliekipiga pia Malindi FC na Timu ya Taifa ya Tanzania na akiwa Meneja wa Taifa stars kwa Miaka 7 Mfululizo
  13. Tuzo ya heshima imekwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa kukuza soka nchini
  14. Ester Adalbelt ni Mwamuzi bora Ligi kuu ya wanawake (SWPL)
  15. Kamishna bora wa soka ni Issack Munisi
  16. Seti bora ya waamuzi ligi kuu Janeth Balama, Tatu Malogo, Joneysia Rukya na Mohamed Mkono
  17. Glory Tesha ni mwamuzi bora msaidizi Ligi kuu ya wanawake (SWPL)
  18. Frank Komba ni mwamuzi bora Msaidizi Ligi kuu ya NBC Tanzania bara
  19. Golikipa bora wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup ni Djigui Diarra kutoka Yanga SC
  20. Mfungaji bora wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup ni Andrew Simchimba kutoka Ihefu Sports Club
  21. Mchezaji bora wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup ni Bakari Nondo Mwamnyeto kutoka Yanga SC
  22. Kocha bora wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara ni Nasredine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga SC
  23. Tukio bora la kiungwana “Fair Play” imekwenda kwa Saido Ntibazonkiza Wa Simba SC katika mechi ya Simba SC Vs Yanga SC
  24. Mchezaji bora chipukizi Ligi kuu Tanzania bara (NBC)  ni Lameck Lawi Kutoka Coastal Union FC
  25. Beki bora Ligi kuu ya Tanzania bara (NBC) ni Dickson Job kutoka Yanga SC
  26. Kiungo bora Ligi kuu ya Tanzania bara (NBC) ni Saido Ntibazonkiza Wa Simba SC
  27. Meneja bora wa uwanja ni Omary Malule, Meneja wa uwanja wa Highland Estate unaotumiwa na Ihefu SC
  28. Golikipa bora wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara ni Djigui Diarra kutoka Yanga SC
  29. Mfungaji bora wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara imekwenda kwa Fiston Mayele wa Yanga SC na Saido Ntibazonkiza wa Simba SC wakilingana wote kwa pamoja kwa Goli 17 Msimu huu wa 2022/23
  30. Goli bora la Ligi kuu ya NBC Tanzania bara Msimu wa 2022/23 inakwenda kwa Fiston Mayele kutoka Yanga SC
  31. Tuzo ya Mchezaji bora, Most Valuable Player (MVP) Ligi kuu ya NBC Tanzania bara imekwenda kwa Fiston Mayele kutoka Yanga SC
  32. Timu yenye nidhamu Ligi kuu NBC Tanzania bara Msimu wa 2022/23 ni KMC FC Kutoka Manispaa ya kinondoni
  33. Kikosi bora cha Ligi kuu ya NBC Tanzania ni  Djigui Diarra (Yanga SC), Dickson Job (Yanga SC), Henock Inonga (Simba SC), Bakar  Mwamnyeto (Yanga SC), Shomari kapombe (Simba SC), Mohamed Hussein (Simba SC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Bruno Gomez (Singida BS), Saido Ntibazonkiza (Simba SC), Clatous Chama (Simba SC) na Fiston Mayele (Yanga SC)

Kwa taarifa zaidi za soka na usajili duniani, endelea kutufuatilia hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version