Ukitazama timu nyingi katika michuano ya Mataifa barani Afrika mwaka huu inayofanyikia nchini Ivory Coast kuna vijana weni sana ambao wanawatumia katika baadhi ya mechi zao katika michuano hii na hii sio kwa bahati mbaya, bali ni uwekezaji sahihi kuanzia ngazi za chini kabisa mpaka kufikia hatua hii ya kulitumikia Taifa husika.

Ukiitazama timu ya taifa ya Tanzania utagundua kuwa shida yetu kubwa tuliyonayo ni namna gani tunatekeleza matakwa ya matumizi ya timu za vijana kuanzia katika vilabu mpaka kwenye timu ya Taifa. Tunapaswa kutazama ni kwa namna gani tumeweka kanuni na mfumo bora wa kuendeleza soka la vijana.

Tokea Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) imeweka kanuni ya wageni vilabu vyetu vimekuwa kwa kasi kubwa kimataifa. Swali ni je kuna falsafa gani au kanuni gani imewekwa ili kuhakikisha miradi yote ya vijana katika kuanzia ngazi ya klabu inafana na kuwa na mwendelezo sahihi?

Tatizo ni kubwa kwani uwekezaji unahitajika sana, ukitazama  mataifa yanayofanya vizuri yaliwekeza, na hata kama hayakufanya hivyo yanatumia fursa ya wachezaji wake kukulia mataifa yaliyowekeza, sisi bado tunashida hakuna kitu tunaweza zaidi ya kuombana kuchangia timu za taifa hilo lina athari kubwa

Ukitazama hata katika matumizi ya vijana unaona kuwa hakuna mwendelezo,Mfano leo unampeleka Morris Abraham akapate uzoefu lakini utashangaa kocha ajaye hamuiti kikosini, utashangaa kila timu ya Taifa inapoitwa wachezaji wanabadilika kila siku, vijana ndo hawaeleweki  kabisa leo anaitwa Clement anacheza dk 90 mechi muhimu kesho anaachwa.

Kuna wakati mwingine unajiuliza tumerogwa au tumeamua kuwekeza zaidi kwenye siasa badala ya uwekezaji rasmi wa miundombinu ya michezo na kuwavutia wazazi na vijana wengi kujiunga katika majukwaa hayo?

Tatizo ni kwamba sera za kusimamia michezo tunazo lakini hazitekelezeki leo hii ukitaka kujenga kituo cha kulea watoto wajifunze michezo hizo kodi utakazolipa, wazazi hawana mpango wa kulipiia watoto wao wakawe wanamichezo kutokana na changamoto kama hizi.

 

SOMA ZAIDI:Makocha Wazawa Ndio Uhai wa Taifa Stars kuelekea Mafanikio

 

Leave A Reply


Exit mobile version