Mengi yamekua yakijadiliwa na kuzungumzwa katika vijiwe mbalimbali vya soka nchini Tanzania haswa baada ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuanza vibaya michuano hii kwa kipigo kutoka kwa wana nusufainali wa kombe la dunia, timu ya taifa ya Morocco.

Wakati hayo yanaendelea tunapaswa kufahamu kuwa kwa sasa ni wakati rasmi wa kusahau kuhusu kipigo hicho na kujifunza kuhusu wapi tulikosea ili kuhakikisha kuwa tunaondoka na ushindi katika mchezo unaofuata ambao ni dhidi ya Zambia.

Ikumbukwe pia mchezo dhidi ya Zambia utakua mchezo wa pili wa hatua ya makundi katika michuano hii ya mataifa barani Afrika n ani moja kati ya mchezo mgumu pia kwani katika kundi ambalo Taifa Stars yupo anakutana na timu ambazo tayari zimekwishawahi kuchukua taji hili ambalo ndio kubwa zaidi kwa ngazi ya timu za Taifa kutoka katika bara la Afrika.

Ingawa kipigo kutoka kwa Morocco kinaweza kuwa changamoto, Taifa Stars inapaswa kuchukua mafunzo kutoka kwa mchezo huo. Kujua ni wapi walikosea na jinsi wanavyoweza kuboresha itawasaidia kusonga mbele na kufanya vizuri katika michezo miwili ya mbele ambayo ni dhidi ya Zambia Pamoja na ule dhidi ya DR Congo.

Ushirikiano ndani ya timu ni muhimu katika kufikia mafanikio. Wachezaji wanapaswa kujenga imani na kuelewana vyema uwanjani. Mazoezi na mazungumzo ya kujenga timu yanaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wao.

Lakini pia mara nyingine, mbinu na mkakati ndio mambo yanayoweza kufanya tofauti na kuleta mabadiliko  kwenye uwanja. Kocha na wachezaji wanapaswa kufanya kazi pamoja kuandaa mbinu zinazofaa kwa mchezo dhidi ya Zambia. Kuelewa udhaifu na nguvu za wapinzani wao ni muhimu.

Siku zote kipigo kinaweza kusababisha hisia za kukata tamaa licha ya kuwa walicheza dhidi ya timu la daraa kubwa zaidi barani Afrika lakini Taifa Stars inahitaji kuweka akili timamu. Kila mchezaji na kiongozi wa timu anapaswa kuwa na mtazamo mzuri na kujitolea kufanya vizuri katika michezo inayofuata.

Mchezo dhidi ya Zambia ni fursa mpya kwa Taifa Stars kuonyesha uwezo wao na kurejesha heshima. Ni muhimu kwa wachezaji kujitathmini binafsi, kuweka lengo la ushindi, na kufanya kazi kwa pamoja kufikia malengo hayo. Kwa kufanya hivyo, wanaweza kuendelea kuwa na matumaini na kushinda michezo ijayo ya AFCON.

SOMA ZAIDI: Kadi Nyekundu Kwa Novatus Ni Njia Ya Kujifunza Kwetu

2 Comments

  1. Pingback: Zingatieni Haya Wanasimba Mabadiliko Ya Katiba - Kijiweni

  2. Pingback: Msimlaumu Onana, Senegal Wana Timu Bora Sana - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version